Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
iko wazi kwamba yeye ndiye kiongozi wa juu kabisa wa majeshi yote nchini.
Swali langu ni dogo tu , ni lini Mheshimiwa atavaa sare za polisi ili kuonyesha kuunga mkono juhudi zao za kupambana na uhalifu au ni lazima avae za JWTZ tu kama ambavyo ameonekana mara kadhaa?
Naomba kuwasilisha.
====
Maoni ya Wadau
Unauliza ili ujue au ili uzonge?
Mpango mzima wa utawala wa kidemokrasia ni mpango mgeni kwetu Tanzania.
Hili la civilian leadership of the military, katika mazungumzo ukilitaja, unaweza kuambiwa "wewe mbona una mind vitu vidogo hivyo?"
Mkapa kakubali CCM wametumia hela za EPA kwenye uchaguzi. Katika kitabu cha kuelezea maisha yake. Na hamna anayemshitaki wala kuanzisha tume ya uchunguzi. Ndiyo kwanza Zitto Kabwe, mwanasiasa maarufu wa upinzani, anamsifia Twitter huyo Mkapa kwa kuandika kwamba yeye Zitto Kabwe amependa sana jinsi Mkapa alivyokuwa mkweli. Utaambiwa "wewe unalalamika rais anavaa magwanda ya jeshi?"
Tumezoea uchifu chifu. Anachosema mkubwa hakiwezi kuwa kosa.
Ndiyo maana habari za demokrasia, bunge la uwakilishi wa wananchi, mihimili mitatu kukinzana, siasa za vyama, ilani za uchaguzi, siasa za sera, chaguzi zenyewe, elimu rasmi hii ya kupewa vyeti, na nyingi zinazofanana na hizo zinakuwa maigizo tu.
Tukirudi kwenye swali lako la kuhusu "Civilian Leadership of The Military", huko tunakoigiza hii demokrasia, waliona ni jambo la hatari kuchanganya siasa na mambo ya jeshi. Wakajiwekea misingi ya kwamba, jeshi litaongozwa na watu wasio wanajeshi waliochaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi. Wakaweka mipaka kati ya jeshi na uongozi wa kiraia utakaoliongoza jeshi.
Ndiyo maana raisi anakuwa Amiri Mkuu wa Jeshi. Sasa rais kuwa Amiri Mkuu wa Jeshi, ili raia wawe wanaongoza jeshi, na si jeshi linaongoza raia, kimuonekano rais akianza kuvaa migwanda ya jeshi bila sababu maalum, anaondoa muonekano wa raia kuongoza jeshi. Anaturudisha kwenye muonekano wa jeshi kuongoza raia.
Muonekano unatengeneza ukweli wake. Kwenye sheria kuna msemo kwamba, haki si tu itendeke, bali pia ionekane kuwa imetendeka. Kwa sababu muonekano wa haki kutendeka unapanda mbegu ya haki zaidi kutendeka na muonekano wa haki kutotendeka, hata kama imetendeka, unapanda fikra za uonevu.
Vivyo hivyo katika uongozi. Katika nchi ya kidemokrasia, jeshi si tu ni muhimu liongozwe na raia, ni muhimu pia lionekane kwamba linaongozwa na raia. Sio mara tu rais anasema angependa kuwa IGP, mara anasema atawapiga mpaka shangazi za wapinzani, mara kavaa migwanda ya jeshi. Shangazi za wapinzani wengine watakosa raha bure wakijua ndio wanakuja kupigwa sasa.
Sisi Tanzania tulivyokuwa tunaingia kwenye vyama vingi, tuliigiza kulijua hili jambo la "Civilian Control of The Military".
Tukawaambia wanasiasa ambao walikuwa wanajeshi pia kina Kikwete, Ditopile, Makamba, Chiligati, Moses Nnauye na wengine kama hao, wachague moja, siasa ama jeshi. Hao niliowataja wote wakachagua siasa.
Kanuni za "Civilian Leadership of The Military" zikazingatiwa. Kikwete aliyekuwa Kamisaa wa Chama jeshini aliyejua habari hizi, licha ya kwamba alikuwa mwanajeshi, sijawahi kumuona amevaa magwanda ya jeshi kama rais nje ya shughuli za kijeshi. Kwa kweli napata kazi ngumu kukumbuka Kikwete akiwa kavaa magwanda ya kijeshi kama rais wakati wowote.
Sasa Magufuli ambaye jeshi ameishia JKT ya lazima, leo kawa rais, anavaa migwanda kama mtoto aliyenunuliwa nguo ya sikukuu ambaye hawezi kujizuia mpaka sikukuu kuivaa hiyo nguo, ananipa shaka kuhusu uwezo wake wa kuelewa au kujali dhana hii ya "Civilian Leadership of The Military".
Si tu kwa sababu anaipa nchi ambayo inatakiwa kuwa ya kidemokrasia muonekano wa kuongozwa kijeshi, bali pia kwa sababu anatuletea mtiririko mzima wa kurudisha jeshi katika siasa.
Ukweli ni kwamba, rais anaweza kuvaa vyovyote anavyotaka. Anaweza hata kuvaa kibwaya cha wacheza ngoma. Lakini je, muonekano wake utakuwaje?
Magufuli hajaishia kuvaa tu magwanda ya jeshi. Ameteua wanajeshi, na ninapoandika wanajeshi simaanishi wanajeshi wastaafu, namaanisha wanajeshi walio jeshini bado, kushika nafasi za kisiasa serikalini.
Wanaochambua mambo wanajua umuhimu wa ualama (symbolism). Magufuli anaposhobokea magwanda ya jeshi anatupa ujumbe gani?
Ndiyo anataka watu walime kwa meno kwa mwendo wa kijeshi?
Kashaliingiza jeshi kwenye manunuzi ya korosho kusini huko. Kaangusha mapato ya mauzo ya kilimo nje kwa asilimia 55, mwaka uliopita unaoishia Agosti 2019 ukilinganisha na mwaka ulioutangulia. Ripoti ya Benki Kuu ya Oktoba 2019 inaonesha hilo.
Anataka kufuta demokrasia na kuongoza nchi kijeshi?
Anataka kufanya Tanzania iwe nchi ya kijeshi?
Is Tanzania a police state?
The answer lies, at your own gate.