Kumbuka Rais ni Amiri jeshi..kosa likowapi akivaa nguo za jeshi? Au kila anachokifanya Magu ni kibaya? Tuelimike kidogo
Unafahamu "Civilian Control of The Military" ni kitu gani?
Unaelewa kwa nini kina Kikwete, Makamba, Chiligati, Dotopile, Andree Shija, Moses Nnauye waliambiwa wachague moja kati ya jeshi na siasa?
Unaelewa kwa nini Mwalimu Nyerere, rais pekee ambaye ni "Rais wa Vita" Tanzania, hakuvaa magwanda ya jeshi nje ya kuhamasisha vita vya Kagera?
Unaelewa kwa nini Jakaya Mrisho Kikwete, rais oekee ambaye amewahi kuwa mwanajeshi na kamisaa wa siasa jeshini, hakushobokea kuvaa magwanda ya kijeshi akiwa rais?
Unaelewa kwa nini Benjamin William Mkapa, muandiamshi wa habari msomi, mwanadiplomasia wa siku nyingi, na mtu aliyeshika uongozi tangu miaka ya sitini, hajashobokea kuvaa magwanda ya jeshi alivyokuwa rais?
Unaelewa kwa nini Ali Hassan Mwinyi, na hekima zake za Unguja ya zamani, mzee wa Kiswahili, mwanadiplomasia mwenye kujua uwezo wake ulipoishia na kutumia wengine kuongoza, hakushobokea magwanda ya jeshi?
Unaelewa kwamba muonekano wa rais kuvaa vaa magwanda ya kijeshi bika sababu ya kueleweka unaondoa muonekano wa nchi kuendeshwa kidemokrasia na raia?
Umeusoma "Waraka wa Jeshi" na jinsi wanajeshi wanavyokasirika jeshi linavyoingizwa katika siasa?