Ni lini Amiri Jeshi Mkuu atavaa sare za Askari Polisi au Magereza?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


iko wazi kwamba yeye ndiye kiongozi wa juu kabisa wa majeshi yote nchini.

Swali langu ni dogo tu , ni lini Mheshimiwa atavaa sare za polisi ili kuonyesha kuunga mkono juhudi zao za kupambana na uhalifu au ni lazima avae za JWTZ tu kama ambavyo ameonekana mara kadhaa?

Naomba kuwasilisha.

====
Maoni ya Wadau

 
Nadhani mada yako ungeiwasilisha kama ombi,

"Naomba amiri jeshi kuu siku moja avae sare za jeshi la polisi/magereza/traffic/zimamoto/ffu/mgambo, nione jinsi zinavyomkaa vema...."

Lmao[emoji23][emoji23]
Hata hivyo imekaa kama ombi mkuu , japo nilikuwa napenda sana wanasheria waseme kama kuna lolote kikatiba linalohusiana na mavazi haya , lengo kuu ni kujifunza .
 

Avae hayo magwanda ili iweje? Mpate sababu mpya za kumnanga au?

Manake si kwamba akivaa sare za Magereza mtakuja hapa na kuanza kumpongeza....

Sanasana mtakuja na kuendeleza yale yale...’oh oneni huyu, sasa anavaa na sare za Magereza. Kaona zile za jeshi hazitoshi. Sasa anataka kuwa kamishna wa Magereza’

Tokeni hapa na unafiki wenu!
 
Eti hili nalo ni hoja ya kisiasa kwa wafuasi was chadema ambao hawajui hata naana ya vazi la jeshi la ulinzi na usalama (_jw tz),

Mkuu tambua rais anapovaa sare za jw ambayo ina rangi za ugoro =jenzi la magereza ,kaki = jeshi la polisi ,kuna kijani ,ambapo kuna jkt nk.akivaa hivyo basi tambua amevaa sare za majeshi yote ,yaani yeye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote yaliyo inchini ,so akivaa eidha ugoro tu ambayo ni sare ya magereza itakuwa hajafuata protocalli
 
Tanzania dhana ya "Civilian Leadership of The Military" kueleweka vizuri ni vigumu sana.

Sasa naona Magufuli kazidi!

Hii sijui ni mara ya ngapi tu anayavaa hayo magwanda.

Hiyo hapo kwenye video ni leo [11/20/19].

Sina uhakika na mazingira yenyewe [ilikuwa ni kwenye shughuli ya kijeshi? Ya kiraia?].

Kwa muonekano inaonekana kama shughuli haikuwa ni ya kijeshi.

Naweza kuelewa kama shughuli ni ya kijeshi na yeye kama amiri jeshi mkuu labda anataka kuonyesha kuwa yupo pamoja na makamanda wake kwa hali na mali.

Hiyo naweza kuelewa na naweza kuvumilia ikifanyika in small doses.

Ila hapa, hayo magwanda yanahusikaje? Sielewi kabisa. Naona sasa anazidisha mno.

Shughuli inaonekana ni ya kiraia. Magwanda ya nini?

 
Magufuli ni bonge la mshamba, bonge la limbukeni, bado analimbuka mpaka kesho.

Ni kama mtoto umemnunulia nguo ya kuvaa sikukuu, yeye anataka aivae kila siku watu wamuone ana nguo mpya.

Nyerere nimemuona kavaa nguo za kijeshi kwenye harakati za Vita Vya Kagera tu.

Mwinyi sijamuona, Mkapa sijamuona. Kikwete ambaye alikuwa mwanajeshi na anaelewa "Civilian Leadership of The Military", kwa sababu ilimpa uchaguzi wa kuchagua jeshi ama siasa, sikumbuki kumuona kavaa magwanda ya kijeshi kama rais. Anajua walivyoondoka jeshini yeye, kina Makamba, Chiligati, marehemu Ditopile, na wengine wengi, ili wabaki kwenye siasa.

Magufuli limbukeni hajui au hajali hayo.
 
Komredi, kwahiyo ni bora aendelee kuvaa hayahaya ya JWTZ hata kama anaenda kupokea ndege mpya?

Oh sorry naona kama na mimi nimeshamnanga tayari.

Komredi, long time no see! Uko poa?

Hapana. Asiendelee kuvaa hayo ya JW. Maana sasa kazidi. Kwa mfano, hiyo jana aliyavaa kwa kusudi gani? Manake hapo kwa video inaonekana shughuli ilikuwa ni ya kiraia.

Kwenye shughuli labda zilizo za kijeshi na ambazo labda zinafanyika porini porini huko kwenye makambi ya kijeshi, kama Ngerengere, akivaa magwanda naweza kuelewa. Dressing for the occasion.

Sasa pata picha siku akivaa magwanda ya Magereza au Polisi.

Like...seriously? Si atakuwa amewapa watu fimbo ya kumsulubia?

Ila dizaini za Magufuli wala huwa hazijali. Zikiona kuna kitu baadhi ya watu hawakipendi basi ndo zinazidisha sasa ili watu wazidi kukereka.

Si unaona kwa Makonda..

Hapo si ajabu Magu anamwacha tu jamaa ili kukera watu.

Na hayo magwanda si ajabu kayavaa kwa makusudi tu ili kuwakera wanaokereka.

Kama ushamsoma vizuri, Magu ana makusudi sana. Na usikute yupo humu anatusoma vizuri sana.

Ila walau apunguze kuvaa vaa hayo magwanda.

Haipendezi Rais wa kiraia kuyavaa vaa tu hata pasipohusika.
 
Aisee... sasa ni kwamba wanaoyajua haya na wako karibu na mtu huyu unadhani huwa hawamshauri au hashauriki?
Magufuli hashauriwi na washauri wake, yeye ndiye anawashauri.

Walianza kumshauri wachache, watu wakaona huyu Magufuli ukimshauri tofauti na anavyotaka yeye, anakutoa kazini, anamuweka mwingine.

Kama alivyofanyiwa CAG Assad. Kama alivyofanyiwa Lawrence Mafuru. Kama walivyofanyiwa wataalamu wengi tu.

Sasa washauri ambao wanataka kazi zao wameamua kumuacha tu.
 

Source please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…