Baada ya kutamani sana kulitumikia Jeshi la jamhuri kwa muda mrefu na kukosa.
Nikakubali kwamba pengine sijaandikiwa kupata nafasi, nikaamua kurudi kujikita zaidi kwenye Trading na Gambling.
Si haba mambo imenyooka well, maisha yanasonga nafanya ishu zangu bila kuamrishwa na yeyote napata muda mwingi wa kupumzika na familia sasa imeanza kuniheshimu(vikao na ishu mingi lazima nipewe taarifa).
Baada ya maisha kuwa safi sasa baadhi ndugu(wapo maeneo) waliniomba niandae vitu walivyoniambia kisha niwatumie ili niwe miongoni mwa watakaoingia mafunzoni hivi karibuni.
Wamenikera sana na kuniudhi na kutoheshimu maamuzi yangu, maana kipindi nilikuwa nauhitaji nako walijikausha kimya na kunipiga saundi kibao.
Sikutaka kujifikiria wala kupoteza muda wangu tena, zaidi nikatoa jibu kwamba HAPANA. siwezi na sipo teyari kwenda mafunzoni.
Nimeridhika sasa na maisha yangu kwa ujumla na kile chenye nakifanya si haba, na sitamani tena kuajiriwa popote pale.
Niwausie ndugu zangu kama umekosa kitu fulani usihuzunike wala kukata tamaa, maana pengine ridhiki yako ipo pahala pengine. Usije lazimisha kitu fulani hata kama ulitamani sana kukipata ilihali kimegoma kuja kwako, kunjua roho Mungu atakubariki utapata kilichobora na kukustahili zaidi.
Hallelujah!!!