Chotti de Alba
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 348
- 106
Kwa wanafunzi wa vyuoni si jambo geni sana kwa lecturers kuwa na mamlaka ya kufanya wanafunzi wafeli na kujitapa kabisa! Imekuwa kero lakini hakuna pa kuyapeleka.utamwambia nani?mwalinu anakuwa na nguvu ya kusema utarudia somo langu hata mara tano!jaman ni janga
iundwe necta ya vyuo vikuu.
Kwa wanafunzi wa vyuoni si jambo geni sana kwa lecturers kuwa na mamlaka ya kufanya wanafunzi wafeli na kujitapa kabisa! Imekuwa kero lakini hakuna pa kuyapeleka.utamwambia nani?mwalinu anakuwa na nguvu ya kusema utarudia somo langu hata mara tano!jaman ni janga
Kwamba unafaulu halafu anakufelisha au inakuwaje???
Hao watakua malecture wa udsm.
acha uzushi soma kwa bidii utafaulu acha visingizio vya ajabu hizo kes mara nyingi ni kwa watu walioshindwa na huwa hawasom ns wanataka kifaulu
iundwe necta ya vyuo vikuu.
Mkuu naomba nikusaidie/niwasaidie (kwa yeyote atakayehusika) hapa kwa kutoa maoni yangu kulingana na mazingira na mfumo mzima wa maisha ya chuo. Kwa kawaida kila mwanafunzi chuoni hutakiwa kuwa na mshauri wake wa masuala ya taaluma (Academic advisor) na kabla ya muhula kuanza kila mwanafunzi hupangiwa mshauri wake na majina hupelekwa kitivo husika. Mkuu/Mlezi wa kitivo (Faculty Dean) hutakiwa kuwafahamisha wanafunzi wa kitivo chake kuhusu washauri wao waliopangiwa.
Sasa linapotokea tatizo lolote la kitaaluma mwanafunzi hutakiwa kushirikiana na serikali ya wanafunzi ya chuo kupitia ngazi zifuatazo kwa mpangilio wake ili kuweka mambo sawa:
1. Academic Advisor (Uliyepangiwa siku unaanza chuo na una uhuru wa kubadilisha)
2. Head of Department (inakopatikana kozi iliyoleta utata)
3. Dean of Faculty
4. Senate (hapa ndipo maamuzi ya mwisho hufanyika baada ya 1,2 na 3 kushindikana)
Usiporidhika na maamuzi ya Senate hatua inayofuata ni kwenda mahakamani. Hivi ndivyo ninavyoelewa kuhusu utatuzi wa migogoro ya kitaaluma chuoni ila kuna wanaoelewa zaidi na watatuelimisha hatimaye kila kitu kitakwenda sawa.
Nimekuelewa kiongozi na nimeshuhudia mwanafunzi ametongozwa na mwalimu wake akaenda kumshtaki hadi kwa dean na uongozi wa shule yule mwalimu akaitwa akaonywa na yakaisha hapo according to the senate lakini yule binti alikipata cha moto. Lile somo alipata A ila ya walimu wengne kama watatu hv wote wakampa sup tht means walimu wanashirikiana kuwadidimiza wanaowachoma..jamani serikali tusaidieni kuondoa mamlaka ya waalimu vyuoni hata kwa kuweka external markers wa mitihani yote.
Mkuu najua kuna mikwaruzano mingi vyuoni kati ya wanafunzi na wahadhiri wao na matukio kama hayo (wasichana kutongozwa) hutokea. Kwa kufahamu hali hizo ndiyo maana matokeo hupitia hatua nyingi ikiwemo kupitiwa na watahini wa nje (external examiners) kisha senate kuyaidhinisha lakini kabla ya kuidhinishwa na senate lazima zipitiwe rufaa za wanafunzi kwa masomo yaliyokatiwa rufaa. Si hivyo tu bali pia senate hupitia mapendekezo ya watahini wa nje (external examiners recommendation review and implementation) na baada ya kujiridhisha ndipo matokeo huwa rasmi.
Lakini pamoja na yote hayo bado kuna baadhi wahadhiri wasiopenda mambo yaende kiurahisi na ndio hao hufikia hatua ya kutisha wanafunzi na kuwajengea hofu hatimaye kuwafanya wasijiamini na matokeo yake ndiyo hayo kufeli/kufelishwa.
Ifike mahala wanafunzi wafuate taratibu na sheria za chuo zinazowaongoza, hali kadhalika wahadhiri nao (baadhi) wenye kujiona wao ndio "NECTA ya chuo" wabadilike na wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu na kanuni zinazowaongoza.
Lakini ili kuweka mazingira sawa mimi naona serikali iweke NECTA ya Vyuo japo ni ngumu ila itasaidia sana.
DAWA moja kigongo sana kwa lecturers wasumbufu ni kuhakikisha unafanya yafuatayo:
1. Hakikisha unasoma kozi unayoipenda na KUIMUDU.
2. Hudhuria vipindi vyote darasani.
3. Fanya test na assignment zote.
4. Hakikisha unascore 70%+ kwenye test, assignments na paper zote (Jisomee na kuelewa unachosoma)
5. Tusikuone Facebook (the greatest time waster for useless people)
ukilenga kufanya hayo HAKUNA lecturer au mtu yeyote atakayekutisha hapa ulimwenguni, achilia mbali duniani.
DAWA moja kigongo sana kwa lecturers wasumbufu ni kuhakikisha unafanya yafuatayo:
1. Hakikisha unasoma kozi unayoipenda na KUIMUDU.
2. Hudhuria vipindi vyote darasani.
3. Fanya test na assignment zote.
4. Hakikisha unascore 70%+ kwenye test, assignments na paper zote (Jisomee na kuelewa unachosoma)
5. Tusikuone Facebook (the greatest time waster for useless people)
ukilenga kufanya hayo HAKUNA lecturer au mtu yeyote atakayekutisha hapa ulimwenguni, achilia mbali duniani.