Ni lini lecturers watapunguza mamlaka ya kuamua mwanafunzi gani afaulu na yupi afeli

Chotti de Alba

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2013
Posts
348
Reaction score
106
Kwa wanafunzi wa vyuoni si jambo geni sana kwa lecturers kuwa na mamlaka ya kufanya wanafunzi wafeli na kujitapa kabisa! Imekuwa kero lakini hakuna pa kuyapeleka.utamwambia nani?mwalinu anakuwa na nguvu ya kusema utarudia somo langu hata mara tano!jaman ni janga
 
Kwamba unafaulu halafu anakufelisha au inakuwaje???
 
acha uzushi soma kwa bidii utafaulu acha visingizio vya ajabu hizo kes mara nyingi ni kwa watu walioshindwa na huwa hawasom ns wanataka kifaulu
 
Mkuu naomba nikusaidie/niwasaidie (kwa yeyote atakayehusika) hapa kwa kutoa maoni yangu kulingana na mazingira na mfumo mzima wa maisha ya chuo. Kwa kawaida kila mwanafunzi chuoni hutakiwa kuwa na mshauri wake wa masuala ya taaluma (Academic advisor) na kabla ya muhula kuanza kila mwanafunzi hupangiwa mshauri wake na majina hupelekwa kitivo husika. Mkuu/Mlezi wa kitivo (Faculty Dean) hutakiwa kuwafahamisha wanafunzi wa kitivo chake kuhusu washauri wao waliopangiwa.

Sasa linapotokea tatizo lolote la kitaaluma mwanafunzi hutakiwa kushirikiana na serikali ya wanafunzi ya chuo kupitia ngazi zifuatazo kwa mpangilio wake ili kuweka mambo sawa:

1. Academic Advisor (Uliyepangiwa siku unaanza chuo na una uhuru wa kubadilisha)

2. Head of Department (inakopatikana kozi iliyoleta utata)

3. Dean of Faculty

4. Senate (hapa ndipo maamuzi ya mwisho hufanyika baada ya 1,2 na 3 kushindikana)

Usiporidhika na maamuzi ya Senate hatua inayofuata ni kwenda mahakamani. Hivi ndivyo ninavyoelewa kuhusu utatuzi wa migogoro ya kitaaluma chuoni ila kuna wanaoelewa zaidi na watatuelimisha hatimaye kila kitu kitakwenda sawa.
 
At some point ndio ..unakuta mwanafunzi anastahili marks flani bt lecturer akiwa na malice nae anampa marks anazotaka yeye na kinachouma zaidi hakuna wa kumlalamikia coz at the end ni yeye ndo anaedetermine maisha yako ya chuo
 
acha uzushi soma kwa bidii utafaulu acha visingizio vya ajabu hizo kes mara nyingi ni kwa watu walioshindwa na huwa hawasom ns wanataka kifaulu

Labda ulipokuwa unasoma wewe hawakuwa hivyo bt alievaa kiatu ndo anajua kimembana au la.hadi nimeamua kuchagua course nnayosoma ni kwamba naipenda na naiweza hivyo swala la kufaulu au kufeli haihusiani na mwalimu kujitapa kwako kwamba utarudia somo lake hata mara tano! I just don knw how 2 xprec thc ila ndo ivo
 
iundwe necta ya vyuo vikuu.

Sana tena naiomba serikali iliangalie swala hili kwasababu hata ukilalamika na ukasahishiwa mtihani wako bado anausahisha ni yuleyule na akitoka hapo anakuja kujitapa
 
Mkuu naomba nikusaidie/niwasaidie (kwa yeyote atakayehusika) hapa kwa kutoa maoni yangu kulingana na mazingira na mfumo mzima wa maisha ya chuo. Kwa kawaida kila mwanafunzi chuoni hutakiwa kuwa na mshauri wake wa masuala ya taaluma (Academic advisor) na kabla ya muhula kuanza kila mwanafunzi hupangiwa mshauri wake na majina hupelekwa kitivo husika. Mkuu/Mlezi wa kitivo (Faculty Dean) hutakiwa kuwafahamisha wanafunzi wa kitivo chake kuhusu washauri wao waliopangiwa.

Sasa linapotokea tatizo lolote la kitaaluma mwanafunzi hutakiwa kushirikiana na serikali ya wanafunzi ya chuo kupitia ngazi zifuatazo kwa mpangilio wake ili kuweka mambo sawa:

1. Academic Advisor (Uliyepangiwa siku unaanza chuo na una uhuru wa kubadilisha)

2. Head of Department (inakopatikana kozi iliyoleta utata)

3. Dean of Faculty

4. Senate (hapa ndipo maamuzi ya mwisho hufanyika baada ya 1,2 na 3 kushindikana)

Usiporidhika na maamuzi ya Senate hatua inayofuata ni kwenda mahakamani. Hivi ndivyo ninavyoelewa kuhusu utatuzi wa migogoro ya kitaaluma chuoni ila kuna wanaoelewa zaidi na watatuelimisha hatimaye kila kitu kitakwenda sawa.

Nimekuelewa kiongozi na nimeshuhudia mwanafunzi ametongozwa na mwalimu wake akaenda kumshtaki hadi kwa dean na uongozi wa shule yule mwalimu akaitwa akaonywa na yakaisha hapo according to the senate lakini yule binti alikipata cha moto. Lile somo alipata A ila ya walimu wengne kama watatu hv wote wakampa sup tht means walimu wanashirikiana kuwadidimiza wanaowachoma..jamani serikali tusaidieni kuondoa mamlaka ya waalimu vyuoni hata kwa kuweka external markers wa mitihani yote.
 
Mkuu najua kuna mikwaruzano mingi vyuoni kati ya wanafunzi na wahadhiri wao na matukio kama hayo (wasichana kutongozwa) hutokea. Kwa kufahamu hali hizo ndiyo maana matokeo hupitia hatua nyingi ikiwemo kupitiwa na watahini wa nje (external examiners) kisha senate kuyaidhinisha lakini kabla ya kuidhinishwa na senate lazima zipitiwe rufaa za wanafunzi kwa masomo yaliyokatiwa rufaa. Si hivyo tu bali pia senate hupitia mapendekezo ya watahini wa nje (external examiners recommendation review and implementation) na baada ya kujiridhisha ndipo matokeo huwa rasmi.

Lakini pamoja na yote hayo bado kuna baadhi wahadhiri wasiopenda mambo yaende kiurahisi na ndio hao hufikia hatua ya kutisha wanafunzi na kuwajengea hofu hatimaye kuwafanya wasijiamini na matokeo yake ndiyo hayo kufeli/kufelishwa.

Ifike mahala wanafunzi wafuate taratibu na sheria za chuo zinazowaongoza, hali kadhalika wahadhiri nao (baadhi) wenye kujiona wao ndio "NECTA ya chuo" wabadilike na wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu na kanuni zinazowaongoza.
Lakini ili kuweka mazingira sawa mimi naona serikali iweke NECTA ya Vyuo japo ni ngumu ila itasaidia sana.
 
DAWA moja kigongo sana kwa lecturers wasumbufu ni kuhakikisha unafanya yafuatayo:
1. Hakikisha unasoma kozi unayoipenda na KUIMUDU.
2. Hudhuria vipindi vyote darasani.
3. Fanya test na assignment zote.
4. Hakikisha unascore 70%+ kwenye test, assignments na paper zote (Jisomee na kuelewa unachosoma)
5. Tusikuone Facebook (the greatest time waster for useless people)
6. Kila dakika jikumbushe mstari huu: "hapa chuo/shule nimefuata masomo"

ukilenga kufanya hayo HAKUNA lecturer au mtu yeyote atakayekutisha hapa ulimwenguni, achilia mbali duniani.
 
Well said..
 
DAWA moja kigongo sana kwa lecturers wasumbufu ni kuhakikisha unafanya yafuatayo:
1. Hakikisha unasoma kozi unayoipenda na KUIMUDU.
2. Hudhuria vipindi vyote darasani.
3. Fanya test na assignment zote.
4. Hakikisha unascore 70%+ kwenye test, assignments na paper zote (Jisomee na kuelewa unachosoma)
5. Tusikuone Facebook (the greatest time waster for useless people)

ukilenga kufanya hayo HAKUNA lecturer au mtu yeyote atakayekutisha hapa ulimwenguni, achilia mbali duniani.

Thanx 4 the advice
 
Mengine yoote ni porojo tu, majibu ya hoja yako hapa.
 
Mkuu mleta mada inaonekana haujui ni hatua zipi hufuatwa na vyuo katika kupitisha matokeo yako kabla ya wewe kuyaona. Kimsingi lecturer hapitishi/kupinga matokea ya mwanafunzi; kazi yake kubwa ni kusahihisha na baada ya hapo hukabidhi mamlaka nyingine matokeo yako zenye mamlaka ya kuyajadili na kuyapitisha. Mamlaka hizi hutofautiana kati ya chuo na chuo japo kuna kufanana pia. Kwa mfano, kwa wale waliosoma udsm, baada mwalimu kutunga na mtihani wake kufanywa anaweza kusahihisha mwenye au ikasahihishwa kiidara na wanaidara wote. Matokeo yakitoka huenda kwa department examinar's booard ambao huyapitia matokeo ya mtu mmoja mmoja kabla ya wao kuya approve na kupelekwa faculty examina's board na faculty board. Nao hapa huyapitia na kuyaruhusu yaende kwa undergraduate/postgraduate senate board ambao nao huyapitia na wakijirithisha na kila kitu huruhusu matokeo yaende senate. Senate ndio chombo cha mwisho katika kupitisha matokeo ya wanafunzi na baada ya hapo wanafunzi hupewa. Katika vyombo vyote hiv, mijadala ni mikubwa sana na bahati nzuri katika kila board kuna uwakilishi wa wanafunzi na niseme hakuna watu wanaosikilizwa katika hizi board kama wawakilishi wa wanafunzi. Ninayeyasema haya niliwahi kuwa miongoni mwa mwakilishi wa wanafunzi; tatizo kama viongozi wenu wanafunzi ni wabovu wasiojua matatizo kama hayo unayoyasema basi kelele kama hizi kwa wanafunzi ni kawaida sana.

Ushauri
Wanafunzi wawajibike katika masomo yao na kuondoa dhana ya kuonewa na malecturer. Pia wanafunzi viongozi watumie nafasi zao vizuri kiungozi na hakika hakuna atakaye onyesha kuonewa na mwalimu wake.
 
Hayo yote unayasema na hizo process wanafunzi na waalimu wote wanazijua sasa kwanini mwalimu ajitape kwa mwanafnzi kuwa ana mamlaka ya kuamua ufeli ni uonevu
 
Back
Top Bottom