Ni lini na wapi Mbowe, Zitto, Tundu Lissu & Co walialikwa popote Dunia hii?

Ni lini na wapi Mbowe, Zitto, Tundu Lissu & Co walialikwa popote Dunia hii?

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Naona CHADEMA wamemualika Bobi Mpinzani Mkuu kutoka UG kama mgeni rasmi, najiuliza kwa nini wao akina Mbowe hawaalikwi au ni lini waliwahi kualikwa popote na kuwa wageni wa heshima?

Watanzania sisi ni watu wa kujipendekeza sana, ukiachilia kwa Mbowe kujipeleka kwa Raila Kenya na kupiga naye picha, hawajawahi kualikwa popote pale rasmi na kupewa heshima kama wao wanavyotoa heshima yao kirahisi kwa kila mtu, hii maana yake nini ?

Fikiria Chama kikubwa cha Siasa UG au Kenya kifanye Mkutano wake Mkuu na muhimu halafu Mbowe au Zito aalikwe rasmi kama mgeni wa heshima, ingendeza sana, lkn inabakia kuwa wishful thinking.

Acheni kujishisha namna hiyo, jithaminini kwanza kabla ya kutegemea kuthaminiwa!
 
Back
Top Bottom