Ni lini nchi yetu itaanza kulipa watumishi kwa masaa badala ya malipo kwa mwezi?

halafu amesahau na kitu kingine kwamba kujituma kwenye kazi ni spirit ya mtu,na wabongo automatically hatuna hiyo spirit.
mbona kenya wanalipwa kwa mwezi na wanachapa kazi vizuri bila ya kusimamiwa na mtu.
mtu akishakuwa mvivu hata umlipe kwa saa au dakika haiwezi kuondoa uvivu wake.
Nchi gani duniani ambako wafanyakaxi Wa serikali hulipwa kwa Masaa badala ya mwisho Wa mwezi? Tupe mfano mmoja tu
Wazo la kijinga tu hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inatakiwa ibadili mfumo mzima wa maisha ya nchi hii na kwa wananchi wake.
Hiyo mambo ya mwisho wa mwezi ni zilipendwa. Tumeshiklia kanuni za mkoloni zile zile kubadilika hatutaki.
Serikali haina plan B miaka nenda miaka rudi.

Sahiv watu wanajifanyia kazi kwa mazoea tu na si kwa kujituma huku wakijua mwisho wa mwezi mshahara utaingia tu.
Badiliko dogo kama hilo nchi inashindwa ndo mana hatuendelei tunabaki kunga'nga'na na wapinzani,huku chama tawala kikiwa hakina mbele wala nyuma.
Kwakweli mfumo wa malipo kwa mwezi hapa bongoland unaruhusu watumishi wengi wa umma 'kuvuna bila kupanda'.

Hourly wages kwa kada nyingi itaongeza productivity na wavivu na wanafiki (kama wasomi feki na wanasiasa) wataumbuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assume kwamba una mshahara wa 540,000/= gross (kima cha kati).

Kwa wiki 45 hours, kwa mwezi 180 to 200 hrs.

Now: 540,000/180 = 3,000 kwa saa (gross).

Ukiweka makato ya PAYE, NSSF, HESLB, NHIF nk net itakuwa around 1,700 kwa saa. Hii itasababisha watu washtuke kwamba wanalipwa kidogo sana.

Maana mtu ukichukua hiyo 1,700 ukazidisha kwa masaa 9 unapata almost 15,300 kwa siku. Imagine, ni business ngapi mtaani unaweza kutengeneza kiasi hiki kwa siku? Mind you, hii ni revenue, siyo profit.
Kumbuka kwenye hiyo15300 huyo mtumishi lazma aende NMB, BOA au CRDB kuikopea. Mkopo wa miaka sita ujue kila siku atakatwa na kubaki na 6400 tu.
 
Malipo kwa saa ni ngumu, kwa sababu ya nature ya kazi na mifumo tuliyonayo, maana ukisema ulipwe kwa saa ina maana saa ambayo hujafanya kazi usilipwe!
 
Hii hii serikali ndo ilipe watu kwa masaa! mbona itapata hasara? hivi unajua kuna watu wanafanya kazi za serikali zaidi ya muda wa kazi tena hadi weekends, je umewaza na hilo
 
Kwa hiyo kama kuna watu wanafanya kazi wikiendi ndo watu wasilipwe kwa masaa kwa sababu zipi? 🤒
 
Been there done that. Hakuna nchi ambayo watu WOTE wanalipwa kwa saa.
Kwa hiyo kama hamna basi na sisi hatuwezi fanya hivo,? Jiulize Kwanini nchi za ulaya ni tajiri na sisi ni maskini
 
Nchi za Ulaya kuwa tajiri si kwasababu wanalipwa kwa masaa.
 
Sijasema ni vile wanalipwa kwa masaa ndo mana ni matajiri.
Nimekuambia ujiulize Kwanini wao na si sisi?
 
Serikali inatakiwa ibadili mfumo mzima wa maisha ya nchi hii na kwa wananchi wake.
Hiyo mambo ya mwisho wa mwezi ni zilipendwa. Tumeshiklia kanuni za mkoloni zile zile kubadilika hatutaki.
Serikali haina plan B miaka nenda miaka rudi.

Sahiv watu wanajifanyia kazi kwa mazoea tu na si kwa kujituma huku wakijua mwisho wa mwezi mshahara utaingia tu.
Badiliko dogo kama hilo nchi inashindwa ndo mana hatuendelei tunabaki kunga'nga'na na wapinzani,huku chama tawala kikiwa hakina mbele wala nyuma.
Maana yake isiwe na mkataba wa kudumu Bali iwe term wise.Itakula kwa serikali maana mtu akijichokea anaacha kujaza mkataba inabidi alipwe chake ajiondekee.Serikali haitathubutu na ikithubutu itajuta maana watu wengi wanefungwa na mkataba wa kudumu na mafao ya uzeeni.
 
Atakayeona ndogo aache akafanye mtaani wengine wataziba ajira zitaongezeka.huku mtaani si mchezo kwa wengi kupata hiyo kiasi. na ndio maana wakipunguzwa kazini au kustaafu wanapata tabu sana huku.

Back
Top Bottom