Ni Jambo linakwaza sana. Unanunua vocha kujiunga na kifurushi unachopenda mara unapata ujumbe kuwa Salio lako halitoshi.
Unafuatilia unaambiwa umejiunga na huduma za kidijitali kama vile "afya call" ,"Tikisa ushinde" n.k.
Huna taarifa na huduma hizo,hujui umejiungaje na wala hujui zinahusu nini,ila pesa zako zinakwenda na kiendacho kwa mganga hakirudi.
Je serikali imebariki huu uhuni wa miaka nenda rudi unaofanywa na Vodacom na mitandao mingine ya simu?
Mbaya zaidi nimejaribu kujiondoa na hizo huduma nimeambiwa "Ombi lako la kujiondoa kwenye Tikisa Ushinde halikufanikiwa Piga *149*83# kujaribu tena."
Huu ni wizi kama wizi mwingine,nadhani ni wakati sasa suala hili likashughulikiwa ipasavyo.