Ni lini Serikali itaondoa/ itamaliza kadhia na mateso ya usafiri wa daladala kwenye majiji makubwa?

Ni lini Serikali itaondoa/ itamaliza kadhia na mateso ya usafiri wa daladala kwenye majiji makubwa?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kuna wakati ukizoea sana shida huwa unaacha kuichukulia kama shida ila inageuka kuwa kama maisha ya kawaida.

Kwenye majiji makubwa hasa Dar, Dodoma Mwanza Mbeya na Arusha majira ya asubuhi na jioni wananchi hupata mateso makubwa sana wanapohitaji kusafiri Kwa kutumia daladala.

Licha ya kuwa Ili kuipanda hiyo gari unahitaji nguvu za ziada, hata humo ndani mmejaa kama gunia za mkaa. Ukweli ni kwamba utaratibu huu sio mzuri wala sio sahihi Kwa jamii iliyostaarabika.

Ninaamini kama serikali ikiwa serious inaweza kumaliza hili jambo. Maana ni jambo linalohitaji utashi tu. Ifike wakati daladala ipakie watu level seat basi.

Haya mambo ya kuvunjana viuno kisa kupanda gari yapitwe na wakati.
 
Dhamira ya kuondoa Kero ya Usafiri kwenye majiji makubwa ni njema,lakini tatizo la serikali ni UFISADI,WIZI & UTAPELI!

Kama hayo mambo serikali haiwezi kuyaacha,kero ya Usafiri kwenye majiji haitokaa iishe!
 
Kuna wakati ukizoea sana shida huwa unaacha kuichukulia kama shida ila inageuka kuwa kama maisha ya kawaida. Kwenye majiji makubwa hasa Dar Dodoma Mwanza Mbeya na Arusha majira ...
Kero hiyo haiwezi kumalizika kwa sababu ilishakosewa tangu hatua za awali kabisa za kukosa Mipangomiji iliyo bora
 
Levo seat abiria wenyewe ndo hawapendi.
 
Mimi kwakweli pamoja na ubahili wangu ila siku kama usafiri wangu binafsi una hitilafu bora nichukue hata bolt kuliko kugombania daladala, huku ninakoishi mara nyingi daladala si za kugombania kwahiyo kama siko na usafiri binafsi mara moja moja huwa napanda daladala kiroho safi tu, usafiri wa bongo sehemu nyingi ni shida tena bora Dar kule Dom ndio kabisa gari haiondoki stand hadi ijae mpaka mlangoni yani hadi konda akose pa kusimama ndio wanaondoka
 
Kila mahali ndg! Dah!
Wao wananunukiana ma V8 mapya kila mwaka, wakipita wanalazimisha tuwapishe, tunawahudumia kila kitu. .... Dahhh!!
Wanasiasa wetu ni wabinafsi
 
20240320_150422.jpg

Usafiri Kwa hapa DAR unadhalilisha Sana watu
 
Serikali naona, wana enjoy wakuona raia wake wakihenyeka,kukanyagana,sukumizana kujambiana kwenye mabasi

Ova
 
Usafiri bora huenda sambamba na mipango miji bora yenye miundombinu inayoendana na idadi ya watu.
Ni asilimia ndogo ya majiji na miji inayopangwa (iwe rasmi au siyo rasmi), na hiyo ni changamoto kubwa ambayo haitapata suluhu kwa urahisi.
Majiji yana njia mbili hadi nne za kuingilia bila barabara za mzunguko, hata ujenge na kuita mwendokasi ni jina tu, shida inabaki pale pale kwa sababu ya idadi kubwa ya watu waelekeao upande mmoja.
 
Sahihi
 
Mimi kwakweli pamoja na ubahili wangu ila siku kama usafiri wangu binafsi una hitilafu bora nichukue hata bolt kuliko kugombania daladala, huku ninakoishi mara nyingi daladala si za kugombania kwahiyo kama siko na usafiri binafsi mara moja moja huwa napanda daladala kiroho safi tu, usafiri wa bongo sehemu nyingi ni shida tena bora Dar kule Dom ndio kabisa gari haiondoki stand hadi ijae mpaka mlangoni yani hadi konda akose pa kusimama ndio wanaondoka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] afu wenyewe wameshazoea, inashangaza mnoo.
 
Mimi naamini wananchi tukiongeza presha Kwa watawala inawezekana tu haya mambo ya binadamu kusafiri kama magunia ya mpunga Karne hiii ni aibu kubwa sana
Kero hiyo haiwezi kumalizika kwa sababu ilishakosewa tangu hatua za awali kabisa za kukosa Mipangomiji iliyo bora
 
Serikali naona, wana enjoy wakuona raia wake wakihenyeka,kukanyagana,sukumizana kujambiana kwenye mabasi

Ova
Aliye Shiba hamjui mwenye njaa tusipowafokea tutaenedelea kusafirishwa kama mafurushi hadi vitukuu vyetu.
 
Back
Top Bottom