Ni lini Tanganyika itaacha kuikalia Zanzibar kimabavu?

Ni lini Tanganyika itaacha kuikalia Zanzibar kimabavu?

Tanganyika yenyewe inakaliwa kimabavu na CCM itaikaliaje kimabavu Zanzibar labda wote kwa pamoja tuilaani na kuikemea CCM iache kuzikalia kimabavu Tanganyika na Zanzibar maana wote tu wagonjwa tofauti yetu ni wodi mmoja yuko BIMA mwingine za walalahoi halafu tunalaumiana tunamwacha mkoloni wetu CCM
 
Samia kuwa muislamu maana yake ni kwamba kwa kuwa waislamu hawapendi dhulma hatakubali kuiona Tanganyika ikiidhulumu Zanzibar kwa kuikalia kimabavu. Hii ndiyoilikuwa hojja yangu. You missed my point somewhat.
Kumbuka kisa cha mkata miti aliyekuwa anatumia shoka ambalo limechomekwa kipande cha mti.

Kuvunja Muungano, mzee Mwinyi alijaribu lakini Nyerere alizima jaribio lake.
Tusubiri tuone mwisho wa huyu mh Samia huenda atafanya kitu.
 
Kila kitu kina mazuri na mabaya yake.
Hata hivyo, mazuri (faida)lazima yawe makubwa kuliko mabaya (hasara).
Hatutakiwi kuangalia upande mmoja tu.
Raia wa Zanzibar wana faida za kiuchumi na kijamii kubwa katika Muungano.
Kelele za kisiasa, vyeo na mamlaka havizidi uzito wa faida za kiuchumi na kijamii kwa raia wote.
Kwani wazanzibar wakipewa uhuru na Tanganyika iliyowakalia kimabavu hawatanufaika kiuchumi na rasilimali walizo nazo mkuu? Huenda una hoja lakini umeshindwa kuiweka vizuri ieleweke.
 
Tanganyika kuendelea kukalia visiwa vya Pemba na Unguja kimabavu hauna tofauti na jinsi Urusi inavyokalia majimbo ya Crimea na Donbas huko nchini Ukraine.

Nawaomba wazanzibar wenye nia ya kupigania uhuru wa Zanzibar kupeleka mashtaka Umoja wa Mataifa kama ikishindikana litumwe jeshi la ukombozi kutoka UN kuja kuikomboa Zanzibar kutoka kwenye makucha ya Tanganyika.

Haiwezekani wapeleke majeshi DRC kupambana na M23 wanaoikalia DRC wakati wao wenyewe wameikalia Zanzibar. Huu ni unafiq wa hali ya juu sana.
 
Kwani wazanzibar wakipewa uhuru na Tanganyika iliyowakalia kimabavu hawatanufaika kiuchumi na rasilimali walizo nazo mkuu? Huenda una hoja lakini umeshindwa kuiweka vizuri ieleweke.
Wazanzibari wameongezewa eneo la kujidai kiuchumi kuanzia visiwani mpaka magharibi, kusini hadi kaskazini mwa Tanzania.

Mojawapo ya faida za Muungano hiyo. Wanaweza kuishi, kugombea uongozi wa kisiasa, kumiliki ardhi, makazi, kilimo, ufugaji, uchimbaji madini na biashara yoyote bila pingamizi lolote kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kisheria.
 
Tanganyika inafaidika Nini na kuikalia kimabavu Zanzibar??

Kuna resources zozote nzibar inanyonywa na Tanganyika??

Mkuu hata isipopata kitu, ni khulka ya mwnaadamu kupenda kumtawala mwenziwe kw akumuendesha na kumpangia.
 
Wakubali zanzibar iwe wilaya ya kibiti au kila mtu afe na chake,kuliko huu upuuzi unaoendelea sasa ivi

yani mkuu wakubali kuwa wilaya ndani ya Tanganyika wakati Tanganyika yenyewe ina hali mbaya kupindukia ya kiuchumi? Acha utani mkuu hata wewe usingelikubali
 
yani mkuu wakubali kuwa wilaya ndani ya Tanganyika wakati Tanganyika yenyewe ina hali mbaya kupindukia ya kiuchumi? Acha utani mkuu hata wewe usingelikubali
Sisi haya makelele tushayachoka wakubali tu au tuvunje muungano
 
Usenge huu! Ivi Zanzibar raisi akatokea bara 1day simtakunywa sumu nyinyi?.
Ukisikiliza kilio cha wazanzibar kuhusu unyanyasaji wanaoupata ndani ya muungano huu usioeleweka, ni kama vile Tanganyika imeikalia Zanzibar kimabavu. Ni ukweli usiopingika kwamba wazanzibar wanapata taabu sana na huu muungano. Tangu Nyerere alipomrubuni Karume na kufanikiwa kuikalia Zanzibar kimabavu, kimekuwa ni kilio kisichoisha a!
 
Back
Top Bottom