Ni lini Tanganyika itaacha kuikalia Zanzibar kimabavu?

Ni lini Tanganyika itaacha kuikalia Zanzibar kimabavu?

Serikali ya TZ kwa kupitia Waziri Mkuu Mzee Pinda ilishathibitisha kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya TZ
Hiyo hapana,pinda alikataa zanzibar sio nchi na alisema siku muungano ukivunjika kuna upande utalia na kusaga meno, wabunge wa zanzibar wakawa wanazomea. Nakumbuka vizuri hii issue
 
Huu utaratibu wa Tanganyika kuiamulia Zanzibar kila kitu ni zaidi ya ukoloni mamboleo.
 
Kwa hiyo mnataka wawe kama Somaliland waliojitenga kimabavu? Baada ya kuonewa na Barre miaka ilee
Lakini hata wao ZnZ bila kuwa na nchi yao kamili wanaweza kutupita kiuchumi wakidhamiria
Ni kuongeza uchumi kwa kasi sana na kuleta hata viwanda vya uhakika
Wamezungukwa na maji mengi na bandari wanazo sasa wanashindwa nini?
Wawili wakubwa wako pande hizo wanakwama wapi?
Tatizo la nchi masikini tumezoea kuomba omba ndio maana hatuwezi kufanya vitu vikubwa
 
Ukisikiliza kilio cha wazanzibar kuhusu unyanyasaji wanaoupata ndani ya muungano huu usioeleweka, ni kama vile Tanganyika imeikalia Zanzibar kimabavu. Ni ukweli usiopingika kwamba wazanzibar wanapata taabu sana na huu muungano. Tangu Nyerere alipomrubuni Karume na kufanikiwa kuikalia Zanzibar kimabavu, kimekuwa ni kilio kisichoisha cha wazanzibar kwa jinsi nchi yao ilivyogeuzwa kuwa koloni la Tanganyika. Ushahidi upo wazi wala huhitaji kufanya utafiti kujua ni kiasi gani wazanzibar wamegeuzwa watwana wa watanganyika. Kila kona ya Zanzibar kilio ni hiki hiki.

Ni bahati mbaya kwamba kilio hiki kimekuwa cha muda mrefu lakini viongozi wa wazanzibar wamegeuka kuwa Chifu Mangungo wa Msovero kwa kukubali kuiuza nchi yao kwa watawala wa Tanganyika kwa sababu ya uroho wa fedha. Yuda alimuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha lakini viongozi wa wazanzibar wameiuza nchi yao kwa mkoloni Tanganyika kwa vipande 3 tu vya fedha. Hivi ni lini Tanganyika itakoma kuikalia Zanzibar kimabavu?

MAONI YANGU
Mama Samia wewe ni mzanzibar na muislamu safi. Waislamu hawapendi dhulma. Tafadhali fanya jambo kuinasua nchi yako kutoka kwenye makucha ya Tanganyika. Au nawe umenogewa na vipande 30 vya fedha na kuwaacha wazanzibar wenzako wakiangamia? Jitihada zako za kuikwamua Zanzibar kutoka kwenye makucha ya mkoloni mweusi (Tanganyika) ndizo zikazotoa mwanga wa Zanzibar kujikomboa kiutawala, kiuchumi na kimaendeleo.

Mungu ibariki Zanzbar, Mungu ikomboe Zanzibar.

Pia soma: Wazanzibar: Muungano unatuumiza, unatupausha!

View attachment 2982736
View attachment 2982739
Kwani wamefungwa kamba? Si wavunje muungano. Hii ndoa haikufungiwa mbinguni.
 
Kwani wamefungwa kamba? Si wavunje muungano. Hii ndoa haikufungiwa mbinguni.
Ndio. Wamefungwa kamba na serikali ya Tanganyika iliyowageuza koloni lao tangu tarehe 26 April 1964.
 
Kwa hiyo mnataka wawe kama Somaliland waliojitenga kimabavu? Baada ya kuonewa na Barre miaka ilee
Lakini hata wao ZnZ bila kuwa na nchi yao kamili wanaweza kutupita kiuchumi wakidhamiria
Ni kuongeza uchumi kwa kasi sana na kuleta hata viwanda vya uhakika
Wamezungukwa na maji mengi na bandari wanazo sasa wanashindwa nini?
Wawili wakubwa wako pande hizo wanakwama wapi?
Tatizo la nchi masikini tumezoea kuomba omba ndio maana hatuwezi kufanya vitu vikubwa
Ndio maana yake mkuu. Serikali ya Tanganyika inarudisha nyuma uchumi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa sana. Hivi wanajisikiaje kuendelea kuikalia nchi ya watu na kudunisha maisha ya Wazanzibar?
 
Back
Top Bottom