Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kwa wataalamu wa historia, sayansi ya jamii, na uchumi, umaskini na kubakia nyuma kwa Afrika ni matokeo ya ukoloni uwe wa kisiasa au kiimani au kiutamaduni kama siyo kijamii.
Kupitia jinai hii, nchi za magharibi na za mashariki ya kati ziliingiza dini na kutuibia mali nyingi huku zikiharibu na kufuta mila zetu za maana. Kutokana na hali hii, Afrika ni kama mbuzi aliyefundishwa na fisi kula nyama na akaanza kuwatafuna watoto wake mwenyewe.
Rejea chuki za kidini, migogoro ya kisiasa baina ya nchi na nchi na uoza mwingine mwingi. Ni Waafrika tu wasiotumia majina yao au tuseme waliopoteza utambulisho wao. Akiitwa Mwafrika, kwa walio wengi mbali na wale walioshikilia mila zao, kabla ya kumuona, ima utajua ni mwarabu au mzungu, mkristo, au muislam.
Ajabu, zaidi ya ardhi, madini, utajiri, na vyakula vyetu, hawa waliotuhadaa kutuibia, wanachukia kila tulicho nacho kuanzia rangi yetu hadi mila zetu. Je ni lini tutawabana lau watufidie vinginevyo tuwapige marufuku kwenye bara letu? Je, kwa uzwazwa tulio nao, tutaweza?
NAOMBA KUWASILISHA WANANGU.