Ni lipi kosa la Lutenant Denis Urio? Au Mimi kuna sehemu nimepitwa?

kendy

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
296
Reaction score
564
Lutenant Denis Urio kwa Sasa anateseka na pande mbili, upande wa Kwanza ni upande watetezi wa Mbowe na washitakiwa wenzake.

Pia upande wa pili ambao unamtesa Leutenant Denis Urio ni upande wa wanaomshitaki Mbowe na wenzake.

Nitaanza na upande wa pili
Hawa iko hivi, kwa mtazamo wa nje Urio anaonekana Yuko salama,lakini kwa jicho la ndani Urio hayuko huru,na kukosa Uhuru ni mateso,kwani urio ni Kama msukule tu anafanyishwa kazi bila ridhaa yake.

Sasa narudi upande wa Kwanza ambao Mimi nashindwa kuelewa kwa Nini watu wanamlaumu Urio?

Urio alimtafutia walinzi Mbowe kwa sababu alikua anawahitaji,

Lakini pia Urio aliwatafutia kazi vijana wake aliowafundisha au marafiki zake waliokua wanapigika kimaisha na kazi za hovyo.

Nisipoelewa Mimi ni kwamba je urio alikwenda kushitaki kuwa Mbowe analindwa na makomado waliofukuzwa? Wakati ni yeye aliewatafuta?

Sasa kulikua Kuna sababu gani kuwatoa kwenye kazi zao na Kisha kuwashitaki?

Ama Kama hakua tayari kumtafutia Mbowe walinzi kwa Nini alikubali?

Kwa kifupi ninachoamini Mimi ni kwwmba, ni kweli Urio alikua Ana Nia njema na huruma kwa Mbowe kutokana na madhira anayopitia.
Pia alikua Ana Nia njema na upendo wa kweli wa kuwatafutia kazi marafiki zake, vijana wake na wanafunzi wake kazi nzuri yenye hadhi inayoendana na taaluma yao, kwa sababu ndani ya Mambo ya ukomando pia Kuna taaluma ya ulinzi wa watu muhimu au maalumu.

Sasa nahisi pengine upande wa pili walipogundua kuwa Mbowe kapata wataalamu wenye uzoefu wa masuala ya ulinzi nadhani hawakupenda,ndipo wakatafuta Nani kawaunganisha,ndipo wakagundua kuwa ni urio.

Sasa kwa vile wananguvu ikabidi Urio alazimishwe kuwa upande wao bila kutaka.

Huwezi kushindana na mwenye nguvu.

Kwa Sasa Urio Yuko mtu Kati, namuonea huruma Sana, kesi ikiisha sijui ataishi vipi.

Bado naamini Urio hakua mtu mbaya kwa Mbowe.

Narudia Tena huenda Kuna kipengele nilipitwa,lakini sioni Kama Urio alikua na Nia mbaya na akina Adamoo.
 
Lutenant Denis Urio kwa Sasa anateseka na pande mbili,
Upande wa Kwanza ni upande watetezi wa Mbowe na washitakiwa wenzake...
Basi utakuwa na uelewa mdogo sana wa Mambo .
 
Kosa la Urio ni kushindwa kusimamia ukweli na kujaribu kusema uongo kisa kulinda ajira na cheo, tunafahamu kuwa Urio hajawahi kwenda kutoa taarifa kwa DCI wala hakupanga kuwaingiza kwenye uhalifu isipokuwa amekubali kuwa mtesi wao.
 
Alichemka kumsaidia kiongozi wa upinzani mtu anayelipwa na fedha za serikali ya ccm.Ili kumsave,akaingizwa kingi kwa kuandaa mpango wa uongo.narudia ,urio alilazimishwa kupindisha dhamira yake ya awali ya kumtafutia ulinzi "HOMEBOY".ikumbukwe jamaa bado anaoneka anaishi kizuizini.
 
Anapitiwa na magari ya mawakili na kurudishwa hoteli ule ni uongo mtupu alipaswa awe muwazi dunia ijue
 
lid
Anapitiwa na magari ya mawakili na kurudishwa hoteli ule ni uongo mtupu alipaswa awe muwazi dunia ijue

walijitahidi sana ku frame hilo likesi,
Changamoto imekuwa ni hawa mawakili wa Utetezi akina kibatala,yaani hawa watoto wameiva sana.wanajua wanachokifanya.

Mwisho wa siku shahidi anashusha heshima zake mahakamani kwa kuonekana ametengenezwa tuu.Sijui kwa mashaidi waliobaki,ila hawa waliopita wote nadhani wanajilaumu kuingia kwenye kesi hii.sasa wafanyeje wakati wamepewa amri.Ndiyo maana wakati mwingine zinapita siku hadi tatu wanatafutiza shahidi.ijapo tuliambiwa tayari idadi ya mashahidi.tulijua wako lined-up.
 
Urio ni mchaga aliyeanua kujitoa ufahamu ili kumuangamiza mchaga mwenzake kisiasa
 
Urio ni komando anaesumbuliwa na uroho wa pesa, madalaka na njaa ndo maana unaona anakuwa muongo muongo hivo.

Huyu angekuwa North korea tayari angekuwa ashakula shaba ya Mr Kim kwa kushusha hadhi ya uimara wa makomando.
 
Huyu Urio ni lazima ashtakiwe kwa kuwaingiza makomandoo wenzake kwenye matatizo bila sababu, kama yeye alikuwa na matatixo na mbowe palukuwa hakuna sababu yoyote kuwa ingiza mkenge akina adamoo
 
Kwa siasa za chuki na ukabila za awamu ya Tano ,ilibidi urio afanye aliyofanya Kwa mana awamu Ile kitendo Cha Mtumishi wa umma kuwasiliana na Mpinzani ilikua ni kujitangazia kifo Kwa mwanajeshi .

Yule inaonekana wazi walimtisha kuwa atakiona Cha mtema Kuni kama ataendelea kuwa na mawasiliano na Mbowe. Makomando ni watu wanaoangaliwa Kwa karibu sana kwenye nchi zilizoendelea na zenye Demokrasia ya kuwafanya watu wote kuwa ni binadamu na sio miungu.

Kwa Afrika Komando anakamatwa na Polisi na kuminywa kipumbavu kabisa Kwa sababu ya kuwa karibu na ndugu yake wa chama kingine kama kilivyo kinachojiita Chama tawala kinachotawala kijeshi kikiongozwa na raia we anaotumia jeshi kupindua sanduku la kura.

Vyama vinavyoingia madarakani Kwa mapinduzi ya kutumiaajeshi Kwa mgongo wa katiba ya Chama kimoja ni hatari kuliko mapinduzi ya kizalendo yanayofanywa na majeshi ya kizalendo. Matokeo ya siasa za Chama kimoja kinachoshika hatamu ni kama yamavyoonekana kutumia majeshi kuzuia shughuli za kisiasa wakati hakuna hali ya hatari Wala madaraka hayakupatikana Kwa mapinduzi .

Siasa zinapigwa marufuku kwenye nchi zenye Tawala za kijeshi.

Je, CCM imeingia madarakani Kijeshi ? Jibu ni ndio!

Kama jibu ni ndio basi Wana uhalali kabisa wa Kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Na pia Kwa sababu CCM iliingia kijeshi madarakani basi Wana kila sababu ya kiwakamata na kuwaweka ndani wapinzani nawanaharakati kijeshi.

Uchaguzi wa 2020 ndio unaoiyumbisha nchi mpaka Sasa. Polisi walitumiaka kuvuruga uchaguzi na kufanya kila ubaya Kwa vyama vya upinzani.

Spika alifanya kila ubaya Kwa ajili ya kukilinda Chama Cha mapinduzi, Magufuli alifanya kila mbinu ili kuua upinzani, Polepole ,Bashiru,Sabaya, Makonda na Hapi walifanya kila ubaya kiwaumiza watanzania wenzetu walioamua kufanya siasa za zao kwenye vyama vingine halali kama ilivyo CCM.

Ubaya wowote uliofanywe kwenye uchaguzi 2020 utalipiwa na Mungu Mwenyewe hapa hapa Duniani bila kujali kuwa mtu aliyeufanya ana cheo Gani.

Ltn . Urio atubu na kusema ukweli ili Karma imsamehe pia. Kumfunga mtu asiye na kosa ni dhambi kubwa sana. Mbowe ni baba wa familia na Kuna watu wengi wanamtegemea. Ni dhambi kuona Mbowe anateseka gerezani wakati majambazi na Wala rushwa wakubwa wanatanua mitaani Kwa Raha zao.

Mbowe sio gaidi.
Urio ndiye anayepaswa kushitakiwa Kwa kupanga njama za ugaidi mana yeye ndiye aliyewafundisha magaidi hao na kupanga mikakati yote na kuchukua pesa na kuwalipa
 
Anapitiwa na magari ya mawakili na kurudishwa hoteli ule ni uongo mtupu alipaswa awe muwazi dunia ijue
Kwani huko dar hakuna waandishi wa uchunguzi wakamfuata hadi hotelini kwake, kujua kama yuko huru au kizuizini?,
Au waandishi huko nao ni njaa kali tu, wanashindwa hata kufuata kwa bodaboda? [emoji44]
 
Kwa siasa za chuki na ukabila za awamu ya Tano ,ilibidi urio afanye aliyofanya Kwa mana awamu Ile kitendo Cha Mtumishi wa umma kuwasiliana na Mpinzani ilikua ni kujitangazia kifo Kwa mwanajeshi...
Makomandoo US wanaishi maisha ya shida sana, wengi wao walio nje ya kazi ni homeless, wanalala verandani,
Urio ushahidi wake sio mbaya kama mnavyojipa matumaini,,, utetezi wasilegee,, mambo yataeleweka Bwire akifanyiwa close examination na mawakili wa serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…