Ni mambo gani ambayo wazee wa kitanzania hujutia na hawataki vijana nao yawatokee?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wakuu. Kawaida ya binadamu umri ukienda huanza kutathmini maisha yao na kuanza kujutia baadhi ya mambo na kusema ninge.

Ni mambo gani ambayo wazee wa kitanzania hujutia sana na wangependa vijana wawe tofauti?

Si wazee tu, hata wewe kama kunajambo unafikiri ulitakiwa kulifanya tofauti unaweza share ili wanaokufuata wafaidike?
 
Watoto wa kike kuolewa wakiwa hawana kipato chao...unamaliza chuo unaolewa..mabinti wajitahidi wasifanye haya mambo...watafute kwanza maisha yao ndo waingie ndoani, sio unaolewa unamtegemea mume tu kwakila kitu! Akifa je?
Akikuolea mke wa pili je?.
Tumieni elimu zenu mlizopewa na wazazi wenu !
 
"Laiti ningejua nisingesapoti kile Chama" alisikika mzee mmoja baada ya kukosa fedha za wastaafu za TTCL.🙄🙄
 
Watoto wa kike kuolewa wakiwa hawana kipato chao...unamaliza chuo unaolewa..mabinti wajitahidi wasifanye haya mambo...watafute kwanza maisha yao ndo waingie ndoani, sio unaolewa unamtegemea mume tu kwakila kitu! Akifa je?
Akikuolea mke wa pili je?.
Tumieni elimu zenu mlizopewa na wazazi wenu !
Mmmmmmhmn huu ushauri umetoa wapi kwanza tuanzie hapo?!
Hivi ndoa kumbe zinawazuia wanawake kutafuta maisha?!

Halafu swali jingine unatafuta maisha then uoe au uolewe?!

Sasa naelewa kwann mabinti wengi sasa hivi hali zao sio nzuri kwenye mahusiano.
 
sio kweli, tafiti zinaonyesha wanawake wengi walioolewa kwamfumo uliouelezea hawakuweza kudumu kwenye ndoa zao kitu kilichowapelekea kupata maumivu makali ya nafsi, si kwao tu hayo maumivu bali hata kwa watoto wao!
 
Ndo nachoweza kuwashauri....wanawake wengi wanakua abusive sana kisa hawana elimu..na wenyewe elimu wananyanyaswa kisa hawana kitu...naishia hapa
 
sio kweli, tafiti zinaonyesha wanawake wengi walioolewa kwamfumo uliouelezea hawakuweza kudumu kwenye ndoa zao kitu kilichowapelekea kupata maumivu makali ya nafsi, si kwao tu hayo maumivu bali hata kwa watoto wao!
😀😀😀..basi kila mtu anawaza anavyoona yeye mm ndo ushauri wangu huo hata nikiwa na binti ntahakikisha ana kitu cha kujishikizA
 
Kila zama na kitabu chake,maisha waliyoishi wazee enzi hizo ni tofauti kabisa na maisha ya sasa,

Huwezi kutumia formula ya zamani ili kuishi maisha ya sasa,

Take life easy and enjoy ur life before it's too late.
 
Usipojitambua ukiwa na miaka Ishirini Na mbili jihesabu Safari yako ngumu Sana kimaisha
hakika, nina mfano wa mzee wangu maisha anayopitia kwa wakati huu sio ya kueleweka ! lakini aliwahi kuwa mkurugenzi wa shirika fulani hivi la serikali ila wanawake bwana!
 
😀😀😀..basi kila mtu anawaza anavyoona yeye mm ndo ushauri wangu huo hata nikiwa na binti ntahakikisha ana kitu cha kujishikizA
lakini umwambie asikiangalie kile kitu anachojishikiza nacho kwa jicho la kwamba akizinguliwa anacho chakumbeba, siku zote ukibeba mawili moja linaweza kukuponyoka muda wowote.
 
Mm nataka na mtoto wa kike akili ichangamke..umesoma lakini upo tu huna chochote cha kufanya kazi kuzaa tu nakulea ...umeagana na Mungu ww? ..hayo ni mengine...!ni ziada
 
Wazeee wengi husema unamuona mtoto wa flani ni mwanajeshi, unaona mtoto wa Fulani ni mwanasheria , unamuona fulani ni Dokta wanasahau hizo Dreams zinatimia kwa uwekezaji mzuri wa kesho
Wengine hulazimisha dreams zao kwa watoto wao.
 
Back
Top Bottom