Ni mambo gani mepesi kufanyika ambayo huwezi kuyafanya?

Ni mambo gani mepesi kufanyika ambayo huwezi kuyafanya?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
1. Kukata chips Kama wanavokata wakaanga chips wanamenya kiazi wwnapiga mistari yao sijui ndo ya diagonal chap vipande vinatokea Mimi nahangaika nitaanza kukata kwenye circle Kwanza ndo circle moja nitoe vipande.

2. Kupiga mlunzi aisee nimeshindwaga

3. Kucheza mziki ni rahisi Ila nishapishana nao naonaga hata Soo kwenye watu wengi kucheza kimasai aisee labda ningekuwaga kwenye team ya dance nikaririshwe zile move Ila me na style yangu moja tu ama mbili za mziki hizohizo naishi nazo sitaki shida.

4. Kufungua kizibo Cha chupa ya bia kwa chupa nyingine..hii kitu imenishinda Nisha jaribu mshikaji wangu yeye akikaa kwenye meza haitaji opener anashika chupa mbili anaziumanisha kwaa moja inaachia sijui huu ujuzi unakuja Kama kipaji ama laa.

5. Kuongea na simu bila kuweka loudspeaker hii Sasa ni tabia imejengeka mpaka naona kuongea bila loudspeaker sikuelewi vizuri labda iwe ishu ya Siri Sana Ila mazungumzo yoyote ya kawaida lazima nikuweke loud
 
  1. Kuendelea kutuma sms wakat za mwanzo hazijajibiwa
  2. Kupost vitu vya maana wasap status
  3. Kujipendekeza kwa wanawake
  4. Kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja kama kuongea na kuandika kitu. Lazima nikosee
 
Kumenya ndizi za kupika kama wachagga ‘wana style yao ya kumeng’enyua ndizi. Hawamenyi ganda la ndizi na kisu

Kukata mboga za majani nimeshikilia mkononi, kama hamna cutting board. Hizo mboga akate mwingine
 
Back
Top Bottom