Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Religion and witchcraft depends on who is doing it.

Kinacho fanyika makanisani hakina tofauti na wanachofanya waganga na wachawi.

Wakatoliki watakushangaa kusali makaburini kwa mababu zako, Lakini hawajishangai wao kusali kwenye zege lililosimamishwa kama sanamu ya bikira Maria na Yesu.
 
Point yako ni ipi mkuu?
 
Kuna kanisa Czech Republic limepambwa kwa mifupa ya watu
1000022939.jpg
1000022940.jpg
1000022938.jpg
 
Hii siyo hadithi wala story ni mwaka huu tu imetokea kwenye kanisa langu la siku zote.

Basi kulikuwa na usimikaji/kuzindua kanisa jipya tulilo changa ma hela kwa miaka kadhaa hadi mwaka huu likawa limekamilika na hatimae Askofu alikuja kulizindua kanisa hilo pamoja na kupewa hadhi ya kuwa parokia

Jambo lililo tuacha midomo wazi waumini wengi ni mambo kadhaa wa kadhaa (sita yataja yote) tukio la kulisimika kanisa lilianza saa3 asubuhi hadi saa10 jioni.

Moja ya matukio tuliyoona kwa macho ni mifupa ya marehemu aliye fariki siku nyingi kuletwa na kuzikwa kweye arutale(mimbari) Huyu marehemu ambaye kwa sasa tunamuita MT fulani kwa imani yetu.

Kulikuwa na chungu kama vile vya waganga wa kienyeji na vilikuwa na vitu kadhaa mle ndani pamoja na mkaa wa moto huku moshi mzito ukifuka.

Baada ya yote hayo kuisha kiongozi wetu wa dini yaani (.....) alipapaka mafuta na kuanza kupasugua na kupasafisha yeye mwenyewe. Na mengine mengi.

Hakika kwa haya yameniacha mdomo wazi na sio mimi tu nimejaribu kuuliza viongozi kadhaa wa dhehebu langu sijapewa jibu la kueleweka maana mimi niliona kama ni kinyume na ukristo.

Wakuu nahitaji kuuliza maana nilijua najua vitu vingi kwenye imani yangu kumbe bado kabisaaa ni mtoto.je hii ina ulazima gani na kwanini ifanyike hadharani na mc akitangaza hadharani kwenye vipaza sauti na watu wasio sali dhehebu letu wasikie na kujua kinacho endelea?

Je, wewe umewahi kuona kitu ambacho kilikuacha mdomo wazi na maswali mengi .
...Hilo Kabisa halina Jina ? Kama ilitokea kweli Kwa Nini unaficha jina la Kanisa ?? Ilikuwa Siri ??...
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.Na masalia yanayowekwa sio ya muanzilishi wa kanisa maana muasisi wa kanisa ni Yesu mwenyewe alipomuambia Petro ya kwamba atalijenga kanisa lake juu yake.

Tukio unalosema ni kutabaruku kanisa.Maana yake ni kuliweka wakfu jengo hilo na kulitenga mbali na shughuli nyingine za kidunia/kijamii ili litumike tu kwa ajili ya sadaka ya ibada takatifu ya misa.

Ubani unawekwa katika chungu na kufukizwa juu ya altare (meza ile ya kutolea dhabihu)ishara ishara ya kupatakatifuza na kumsihi Mungu ya kwamba sadaka zitakazotolewa hapo zipae kwake juu na harufu nzuri ya kumpendeza kama moshi huo wa ubani.Kadhalika husuguliwa kwa mafuta matakatifu ishara ya kupatakasa.

Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa kuwa msimamizi wa kanisa mahalia.Kwa imani yetu sisi wakatoliki watakatifu wanao uwezo wa kutuombea kwa Mungu ndio maana tuna litania ya watakatifu.Hivyo kuweka alama yake katika kanisa husika ni ishara ya kukabidhi usimamizi wa kanisa husika kwake.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki.
Ndio maana nikasema katupiga kamba akitaka aseme yote aliyoyaona na kushuhudia
 
"sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu"

Hayo masalia ni nini?
 
hio mifupa inatoka wapi ? Kwa mfano parokia ya Mt yuda tade, hio mifupa inakuwa ya huyo yuda ? Wanaitoa wapi ? Je dunia nzima makanisa yote ya yuda wana mifupa yake ?? Ufafanuzi kdg mkuu ,
 
Back
Top Bottom