Si kwa nguvu wala uwezo bali ni kwa Roho wa Mungu, Zekaria 4:6
Kuna mambo mengine hakika hatuwezi bila kuwezeshwa na Roho wa Mungu,
Tupo duniani ni kweli, lakini mambo tunayoyaona kwa macho ni matokeo ya mambo yaliopo katika ulimwengu wa Roho.
Liwe jambo jema au baya, jema likiwa linasimamiwa na Roho wa Mungu, baya likiwa linasimamiwa na roho ya shetani.
Na ndio maana tunatakiwa kuomba kila wakati.
Tunaishi na wanadamu na sisi sote kama wanadamu tunakosea, kipimo cha kosa ni vile lilivyomumiza mtu,
Mfano we unaweza kuniambia "mjinga wewe" nikaumia kupita kiasi, huenda nikapoteza hata hali ya kujiamini
kutokana na neno dogo tu hilo.
Kusamehe ni lazima, kwa ajili ya afya ya roho yako, mwili wako na nafsi yako.
Kweli ni ngumu, lakini ni rahisi ikiwa tutamkimbilia Mungu atupe neema ya kuvumilia.
Sina maana hata kama ni mtu ambaye unaweza au inabidi utengane nae kwa sababu ya Amani yako, usifanye hivo
kwa sababu ya msamaha hapana, Kwa sababu kuna hili neno "Marafiki hawawezi kwenda njia moja kama wasipopatana"
Ila Kinyongo, Kisasi sio kizuri. Kinakuumiza wewe mwenyewe na jamii yako.
Najua inavyouma na ilivyongumu, lakini tukitaka kubarikiwa ni lazima kusamehe, na kuwapenda waliotutesa na kutuumiza.
Mimi binafsi nilishapitia katika wakati mgumu wa kumsamehe mtu, ningekuwa na uwezo na kama sio neema ya Mungu ningeweza,
kutafuta wahuni wammalize huyo mtu, nilikuwa naona afadhali asiwepo kwenye huu uso wa dunia bora afe tu.
Lakini wakati ulipofika Mungu aliniwezesha, nikafikiria, dunia yenyewe hii sote tunapita, sawa ndio imetokea hivi, lakini Mungu si anaona,
na ajua ukweli wa moyo wangu, basi, "KISASI NI JUU BWANA"
Nikakiri kwa kinywa changu nimesamehe. Na ninayo furaha na amani, na maisha yanaendelea.
Hata nikikumbuka, huwa namwambia Mungu, Wewe ndiwe mtetezi wangu uliye hai NITETEE amani yangu idumu.
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu, Wafilipi 4:13