Ni mambo madogo madogo ila yanakera sana

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
1. Unaona dumu la maji, unaenda kulinyanyua kwa nguvu ukidhani lina maji kumbe lipo tupu. Unakuwa umetumia nguvu zako bure kabisa, inakera

2. Unaona mtu anakusalimia au kukupungia mkono huku akitabasamu. Na wewe unapokea salamu yake/kumpungia mkono ukiwa na tabasamu pana pia. Lakini sekunde chache baadaye unagundua hakuwa anakusalimia/kukupungia wewe bali mtu mwingine aliyepo pembeni ama nyuma yako. Kwa hiyo unakuwa kama umejipendekeza, inakera.

3. Unahisi kupiga chafya, unajiandaa kwa kwa kuasama mdomo huku ukifumba macho. Chafya inaanza kucheza na wewe, inafanya kama inakuja kisha inarudi, kama inakuja inarudi. Baada ya kufanya hivyo kwa muda kisa inapotea, haiji tena. Kwa hiyo chafya inakuwa imekufanya wewe mjinga, inakera.

4. Ndo umeanza kumung'unya tu pipi bado nzima tu mara inachoropoka na unaimeza kwa bahati mbaya. Imagine unaimeza wakati hata hujafaidi vizuri, unaweza tamani upasue tumbo uitoe ili uile tena, inakera

5. Unataka kupiga chafya tu na si kingine chochote. Unapiga chafya na kamasi pia zinatoka. Kwa hiyo unakuwa umefanya kitu zaidi bila ridhaa yako, inakera.

Na kama huna leso utawakera hadi wengine.
 
Unapiga chafya na ushuzi huoooo unaponyoka inakera sana [emoji125][emoji125][emoji125]
😂😅
Hiyo ndo inaitwa kuua ndege wawili kwa jiwe moja!

Ikitokea hivyo unamalizia na neno "NAUNGA JUHUDI"😜
 
Unaona ardhi unayotaka kupita inamatope sana unaamua kuruka kwingine pakavu. Ile unaruka tu unatitia kabia ndani ya tope kumbe kule ndio kuna tope zaidi.

Unaruka hatua kubwa ili kuyaruka majia halagu unatua ndani ya maji..

Unaruka ukidhani kuna shimo mbele kumbe pote pako plain uliona vibaya (Usiku)

Mtoto anakuudhi sanaaa unamkimbiza umkamate unchape halafu anakushijda mbio..unabaki na mchoko plus plus
 
Hiyo ya tatu ina vice versa yake, unadhani pako plain kumbe shimo. 😂😂😂😂😂😂😂. Alooo, unaweza teguka goti aisee.
 
1. Unaenda chooni kwa pupaa, unafanya mambo yako ukijua kwenye ndoo kuna maji kumbe kuna muungwana alikutangulia akayafyeka yote ile unataka kujiswafi unakuta hakuna hata tone
Ina keraaaa..

2. Umekaa huna hili wala lile mara unahisi kuna sehemu inakuwasha kwenye vidole vyako vya mkono unaanza kujikuna ila unashangaa mbona kama sikuni penyewe na muwasho bado unaendelea mwisho wa siku unamaliza kukuna vidole vyote ila bado kamuwasho kapo inabowaaaa....

3.(wakati ukiwa shuleni) unaamua kupiga round kwenda kumsalimia mshkaji wako wa darasa lingine ile umeingia tu baada ya dk 10 mwalimu anaingia na kiboko anasema wote piteni mbele mpige magoti . Inahuzunishaaa...

4.uko zako magomeni unasubiri gari za kwenda Posta ila zinapita za kariakoo tu
Unazidi kusubiri kama dk 20 haipiti yoyote ya posta , mwisho unaamua upande tu ya kariakoo utaunga mbele kwa mbele. Ile unapanda tu na kwenda kushika bomba siti ya nyuma mara unaona gari ya posta hiyoo inaingia kituoni halafu iko tupu
Agggr inakerra sanaa

5.(Kwa wazee wa Ferry mnaelewa)
Unaskia honi ya ferry inalia kwa mbalii unajikoki kukimbia unafika chap unakata ticket yako ile unakimbia kuwahi
Unapofika tu getini ndio yule askari wa SUMA JKT nae anafunga geti
Daah halafu pantoni inatuliaa kama dk 5 ndio inaondoka inabidi uisindikize kwa macho tu
Daaah inakera balaaa..

6. Kigeto geto unaamua kujifurahisha mwenyewe unapita zako gengeni unanunua Parachichi safi kabisaa unaenda nalo ghetto ili ukalilie wali maharage fresh
Unafika unakula wali wako vizuri kabisaa ile umeshamaliza kama dk 5 zimepita ndio unakumbuka parachichi ulisahau kulila na liko juu ya mezaa daaah inakeraaa...

7. kigeto geto na wadau tusivyo penda kuosha vyombo , umeamua kujikusanya ukaoshe vyombo vya wiki nzima
Umeaviosha vyoote umemaliza, ile umevirudisha ndani ndio ghafla unaliona sufuria chafu ulilopikia ugali juzi linakutazama tu ,, daah unaweza kulitukana kana kwamba unaongea na mtu[emoji28]

8. Utotoni unatumwa na mama, nenda chumbani mwangu juu ya meza utakuta chanuo uniletee, daah mjomba unajikoki
Mbio mpaka chumbani
Sijui vyumba vya wazazi hua vina sumaku gani mara unafika unasahau ulichotumwa badala yake unaanza kuzubalia kwenye kioo
Ushajisahau kabisa unastukiaa unazinduliwa na bonge la banzi mgongoni
Daah inashtuaa sanaa...

Daah zinatosha acha wadau wengine pia waandike [emoji28][emoji1488]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kuzima simu ili labda uiweke kwenye chaji, kwa bahati mbaya unarestart hivyo inabidi usubirie izime Kisha iwake ndo uizime tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii hunikuta sana wakati natumia PC, yaani huo muda wa kusubiri izime na ijiwashe tena hua nauona ni mrefu kinoma. Halafu ukute umechoka unataka kulala zako....inakera kinoma.
 
1. Unaenda chooni kwa pupaa, unafanya mambo yako ukijua kwenye ndoo kuna maji kumbe kuna muungwana alikutangulia akayafyeka yote ile unataka kujiswafi unakuta hakuna hata tone
Ina keraaaa..

2. Umekaa huna hili wala lile mara unahisi kuna sehemu inakuwasha kwenye vidole vyako vya mkono unaanza kujikuna ila unashangaa mbona kama sikuni penyewe na muwasho bado unaendelea mwisho wa siku unamaliza kukuna vidole vyote ila bado kamuwasho kapo inabowaaaa....

3.(wakati ukiwa shuleni) unaamua kupiga round kwenda kumsalimia mshkaji wako wa darasa lingine ile umeingia tu baada ya dk 10 mwalimu anaingia na kiboko anasema wote piteni mbele mpige magoti . Inahuzunishaaa...

4.uko zako magomeni unasubiri gari za kwenda Posta ila zinapita za kariakoo tu
Unazidi kusubiri kama dk 20 haipiti yoyote ya posta , mwisho unaamua upande tu ya kariakoo utaunga mbele kwa mbele. Ile unapanda tu na kwenda kushika bomba siti ya nyuma mara unaona gari ya posta hiyoo inaingia kituoni halafu iko tupu
Agggr inakerra sanaa

5.(Kwa wazee wa Ferry mnaelewa)
Unaskia honi ya ferry inalia kwa mbalii unajikoki kukimbia unafika chap unakata ticket yako ile unakimbia kuwahi
Unapofika tu getini ndio yule askari wa SUMA JKT nae anafunga geti
Daah halafu pantoni inatuliaa kama dk 5 ndio inaondoka inabidi uisindikize kwa macho tu
Daaah inakera balaaa..

6. Kigeto geto unaamua kujifurahisha mwenyewe unapita zako gengeni unanunua Parachichi safi kabisaa unaenda nalo ghetto ili ukalilie wali maharage fresh
Unafika unakula wali wako vizuri kabisaa ile umeshamaliza kama dk 5 zimepita ndio unakumbuka parachichi ulisahau kulila na liko juu ya mezaa daaah inakeraaa...

7. kigeto geto na wadau tusivyo penda kuosha vyombo , umeamua kujikusanya ukaoshe vyombo vya wiki nzima
Umeaviosha vyoote umemaliza, ile umevirudisha ndani ndio ghafla unaliona sufuria chafu ulilopikia ugali juzi linakutazama tu ,, daah unaweza kulitukana kana kwamba unaongea na mtu[emoji28]

8. Utotoni unatumwa na mama, nenda chumbani mwangu juu ya meza utakuta chanuo uniletee, daah mjomba unajikoki
Mbio mpaka chumbani
Sijui vyumba vya wazazi hua vina sumaku gani mara unafika unasahau ulichotumwa badala yake unaanza kuzubalia kwenye kioo
Ushajisahau kabisa unastukiaa unazinduliwa na bonge la banzi mgongoni
Daah inashtuaa sanaa...

Daah zinatosha acha wadau wengine pia waandike [emoji28][emoji1488]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ya kwanza unaweza hisi Mungu amekutelekeza bila msaada wowote.😀😀😀😀😀😀
 
Unaandaa zako msosi uliomiss kwa muda mrefu ile kutia vikolombwezo unajikuta umezidisha pilipili. Unakula msosi huku machozi, jasho na kamasi nyepesi vinatililika, kwa uchungu inabidi uwe kila tonge unasindikiza na maji. Inaondoa ladha na mshawasa wa msosi ila haina jinsi ni ngumu pia kutupa msosi unaoukubali
 
😂😂 😂 😂 😂 😂
Au unazidisha chumvi, yaani unaweza tamani uloweke chakula kwenye maji ili u 'dilute chumvi.
 
Back
Top Bottom