Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
1. Unaona dumu la maji, unaenda kulinyanyua kwa nguvu ukidhani lina maji kumbe lipo tupu. Unakuwa umetumia nguvu zako bure kabisa, inakera
2. Unaona mtu anakusalimia au kukupungia mkono huku akitabasamu. Na wewe unapokea salamu yake/kumpungia mkono ukiwa na tabasamu pana pia. Lakini sekunde chache baadaye unagundua hakuwa anakusalimia/kukupungia wewe bali mtu mwingine aliyepo pembeni ama nyuma yako. Kwa hiyo unakuwa kama umejipendekeza, inakera.
3. Unahisi kupiga chafya, unajiandaa kwa kwa kuasama mdomo huku ukifumba macho. Chafya inaanza kucheza na wewe, inafanya kama inakuja kisha inarudi, kama inakuja inarudi. Baada ya kufanya hivyo kwa muda kisa inapotea, haiji tena. Kwa hiyo chafya inakuwa imekufanya wewe mjinga, inakera.
4. Ndo umeanza kumung'unya tu pipi bado nzima tu mara inachoropoka na unaimeza kwa bahati mbaya. Imagine unaimeza wakati hata hujafaidi vizuri, unaweza tamani upasue tumbo uitoe ili uile tena, inakera
5. Unataka kupiga chafya tu na si kingine chochote. Unapiga chafya na kamasi pia zinatoka. Kwa hiyo unakuwa umefanya kitu zaidi bila ridhaa yako, inakera.
Na kama huna leso utawakera hadi wengine.