Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Sasa kupokelewa kuna ubaya gani jaman?
 
Hio tabia wanawake wengi wanayo na sio tabia ya kujivunia. Ni aina flani tu ya mapuuza ambayo wengi mnayaendekeza. Simu unapigia ni urgent issue hupokei. Maana yake ni nini sasa.
 
Kusema kweli sijaona mapungufu mengi kwenye malalamiko yako. Zaidi nimeona mengi ya kumpa hongera.
 

Mkuu yani wife wangu hama time na mimi yani mara zote yeye sa3 kalala mimi huwa nalala sa8 au9 yani hana hata hofu!!! Kuna siku nimemuangalia dada msaidizi wetu nikaanza kumuona kama ni mzuri hivi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nikalikataa hili pepo maana nimeshaapa sitakuka nitembee na dada wa kazi
 
Sijui kwa wengine yanakujaga na midawa. Enzi hizo ilikuwa wanatii. Mwanaume na wewe unajistukia unanyenyekea. Sasa hivi,yanaona bora yakupelekeshe sasa. Ndo maana mababu zetu walikuwa wanaamua kuongeza mke. Ukizingua tu,anahamia kwa bi mdogo wewe unabaki na jeuri yako.
Bi mdogo anashukuru kaolewa,hataki kupoteza bahati. Mkubwa nae akiona keshalikologa, anakuwa mpole asiachwe.
Ya leo hii,hamna kitu.
Kuachwa, haina shida.
Mara,we si kitindamimba kwa wanaume.
Mara ohh,mi nimechoka sitaki.


Kama hayupo kwa kukuzalia kwa mkataba,mlete kwa sharti. Kama una nyumba kubwa, kila mtu na chumba chake. Kama chumba mnalala kimoja,kila mmoja na kitanda chake. Mwanaume unajengaje mazoea ya kulala na maanamke?
 
Mpaka sasa ni hasira tu na namna ya kuzidhibiti.

Akikasirika hataki kuongea, ni mpaka hasira zake ziishe sasa mimi hivyo siwezi. Nataka tuongee kwa wakati huohuo nihakikishe yuko sawa ndipo nami nipate amani.

Na akikakisirika zaidi ndio simpati kokote, na hivi yuko mbali nateseka kummiss, naumia sana.

Ila ndio nampenda jamani, akiweza kubadili hili atakuwa ameniokoa sana.
 
Ongea na wife vizuri tu, sometimes mood zinakua down ujue, after sometimes atakua sawa, achana na mchepuko huko unaweza ukaharibu zaidi[emoji848]

Wife sio muongeaje kabisa yani kuna muda namuonaga ana kiburi cha uzima!!! Yani kama leo kaamka asubui subui eti kaalikwa mgeni kwenye graduation, namwambia wewe lala bwana anasema ngoja niende wataona nimewapuuza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwaiyo bora anipuuze mimi!!! Huyu dawa yake nipte demu mkali zaidi yake ndo akili zitakaa sawa
 
Nimekuelewa vizuri tu, unajua sometimes kuna matendo ya upendo mtu unaweza mfanyia mwenzi wako ila kumbe ukawa unaonekana unajipendekeza au mshamba flani. 🀣
No, tatizo lake ni kuwa lazima aniweke stend, ulishawahi kaa stend/airport dakika 20 kumsubiri mtu, unakuwa unazubaa zubaa kama umepotea. halafu sio mara moja ni recurring.

Mfano ndege ya masaa mawili na nusu si unajua kabisa huyu atatua muda fulani kwanini asiwahi nimkute lazima mimi nimsubiri. Na wala hajawahi ona hili kama tatizo. Kwa ujumla tu ana mapuuza kwenye hili.
 
Hio tabia wanawake wengi wanayo na sio tabia ya kujivunia. Ni aina flani tu ya mapuuza ambayo wengi mnayaendekeza. Simu unapigia ni urgent issue hupokei. Maana yake ni nini sasa.
Binafsi nakuwaga sipo bize sana na simu,

Kwasasa nimejifunza, sikai mbali na simu labda iwe haina chaji,


Na mama bora akupigie usipatikane lkn kuliko usipokee.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Lakini mkuu kwenye hili unamuonea.
 
Sasa wewe dawa ni kumdanganya ushafika ilihali ndio uko angani 🀣 ili muende sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…