Ningetaja lakini haitasaidia mfano kama ndio una million 5 za kununua mashine za kununua tofali, ili hela yake uione lazima atleast uwe na canters za kubeba tofali watu wanataka free delivery ukitegemea gari za kukodi hutatoboa. Nikikwambia mashine za kunyoa ufungue Barbershop unakuta hizo mashine ni kama 5% tu ya vitu vinavyohitajika, za miwa unahitaji premium location kwenye mzunguko mkubwa wa watu na hapo inabidi umtoe mtu au bonge la kishika uchumba, bila ya kujua plan yako ni ngumu kujua tukusaidie nini, na jee unataka kuziendesha mwenyewe au utaajiri watu na wewe uendelee na majukumu yako huko halmashauri maana utakuja kuuza scraper tu kama hakutakua na usimamizi wa karibu...kama vipi jiunge na watanzania wenzako kwenye mashine ambayo return yake ina uhakika sana yani bodaboda ukiwa na nidhamu majanga yanaweza kukuepuka na kufikisha malengo yako.