Ni matumaini yangu Uongozi wa Simba SC umeshaandaa Barua ya Kumfuta Kazi Kochwa wa Hovyo Pablo Franco wa Real Madrid ya Tandale

Ni matumaini yangu Uongozi wa Simba SC umeshaandaa Barua ya Kumfuta Kazi Kochwa wa Hovyo Pablo Franco wa Real Madrid ya Tandale

Penati anakosa Ronaldo,(Bruno jorgino) Salah sembuse Baka, unaonekana sio mpenz wa mpira ila mshabiki tu. Alichokuwa anafanya Inonga ni kuwakumbusha wenzake wawe mchezoni ambacho ni kitu cha kawaida kufanywa na mchezaji anajielewa hasa ukiangalia yeye ni beki wa mwisho hata ukiangalia goli walilofungwa ni uzembe wa M Hussein kushindwa ku mark mfungaji aliyepiga free header, na sio Inonga tu hata Manula huwa anawawakia sana mabeki zake kwahiyo hakuna cha ajabu hapo.

Acha kujifanya mjuaji huna unachokijua kwenye mpira zaidi ya kutafuta sifa tu.
 
Nilishasema katika moja ya Mada ( Threads ) zangu hapa JamiiForums kuwa hakuna Kocha hapa na kutoa sababu zangu kadhaa za Kiufundi na Kiuchambuzi nasikitika Sikueleweka na Kutusiwa na Wadau.

Unajua kabisa kuwa Principle Kuu ya Wapiga Penati ni Kwanza kuanza na wale Mafundi wa Kupiga kama Shomary Kapombe na siyo Wabovu kama Mkude na Inonga.

Kocha mwenye Akili ( ambazo Tapeli wa Kihispania ) Pablo Franco Martin hana pale hasa ilipofika tu hatua ya Mikwaju ya Penati angeanza na Shomary Kapombe, Mohammed Hussein Tshabalala, Meddie Kagere, Pascal Wawa na Saido Kanoute.

Kama Kocha Mkuu umeshaona tokea mapema tu Jonas Mkude anagombana na Mwamuzi mara kwa mara pamoja na Beki Henock Inonga ambaye muda wote ni Kukasirika na Kuwafokea tu Wachezaji wenzake akijifanya anajua Mpira Tanzania nzima wakati Kiuhalisia ni wa Kawaida sana kupelekea Wawili hawa kutoka Mchezoni mapema halafu bado nikashangaa kuwaona nao Wamejumuishwa katika Wapiga Penati zile.

Tafadhali Uongozi wa Simba SC upesi sana Fukuzeni Kocha Mkuu Pablo Franco Martin na Msaidizi wake Suleiman Matola pamoja na Meneja wa Timu Patrick Rweymamu na mtafute Kocha wa muda huku mkimtafuta Kocha Mkuu Mpya anayeendana na Matakwa, Sera na Falsafa za Simba SC.
we jamaa nilijua unazungumzia kocha kuanza na mabeki sita na viungo wakabaji wawili. halafu offensive wawili tu..

kumbe unazungumzia mapigo ya matuta ambayo huwa ni bahati tu. labda ungesema kuwa Nyoni alitakiwa kuingia dakika za nyongeza zile 4 ili aje apige tuta... halafu ukizungumzia kuwa angepiga fulani na fulani sio sawa, penati hupigwa na aliye tayari kupiga. je kama kocha aliuliza kuwa nani yuko tayari kupiga akina mkude wakajitokeza. na ukisema mafundi ndio wanaanza, nakataa. Mara nyingi tu Ureno wanatolewa kabla Ronaldo hajapiga tuta, maana yake anasubiria kupiga mwishoni. Mwisho kabisa 2012 UEFA fainali upande wa chelsea alianza Mata ambaye hakuwa mpigaji mzuri na akakosa, lakini mwisho wa siku waliofuata wakafunga....
 
Nafkiri msimu ujao utatuma maombi ya ualimu hata Simba C ukajionee ukubwa wa kuwamiliki watoto na waende utakavyo
 
Back
Top Bottom