Ni mawazo yamenizidi au uzembe?

Ni mawazo yamenizidi au uzembe?

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Juzi Jumatano nilikua namnunulia mtu voucher kwenye Max malipo ya elfu 10 nikakosea namba ikaenda kwa mtu mwingine.

Leo asubuhi nilikuwa namtumia dogo hela nikakosea hapa nasubiri ndani ya hizi siku 3 irudishwe hiyo hela maana ilikua ni hela ya dogo nimepewa na mtu nimpe ikapitishwa kwangu.

Kinachoniuma zaidi ni sasa hivi nilikua nalipia tena king'amuzi nimekosea namba elfu 69 yangu imeenda na maji.

Inawezekana nina mawazo sana bila kujijua ndo maana nakosea sana au nimekua mzembe tu?

Maana hali hii si kawaida kabisa
 
Jaman kati ya ulipokosea hazijanifikia hata kwa bahati mbaya(joking)

Pole mkuu jaribu kupunguza mawazo. Sema mawazo sio uzembe ukijilaumu uzembe utajenga ile hofu ya kufanya mipango ya pesa ukiogopa kukosea.

Am sure kuna kitu kinakusumbua na kukupa hofu,mawazo,kukosa raha jaribu kukigundua ni kipi hicho kisha anza mazoezi ya kusuluhisha tatizo ulilonalo utakua free.

Uzembe huwa haujirudii zaidi ya mara tatu.
 
Kweli toka nikosee kununua vocha basi nikifanya kitu nafanya mara mbili mbili nahakikisha lakini wapi. Kila nikitaka kufanya kitu cha hela naanza kuwaza nisije nikakosea. Sasa hii ya sasa hivi imenikera zaidi maana nimeangalia mara nne jamani na nimekosea.
 
Tatizo liko kichwani, unafanya kitu huku ukiwa unawaza kwamba utakosea.

Kuna kitu kimefanikiwa kukupotezea confidence, bring back your confidence. Be positive, clear up your mind.
Najaribu kuwaza naona kama uko sawa.
 
Back
Top Bottom