Hata sisi tusikate tamaa. Hawa jamaa walipigwa na njaa mpaka wanamuziki wakubwa duniani wakajumuika kukusanya pesa ya chakula. Leo, mashallah mambo sio mabaya.
Lakini pia, Ethiopia ni nchi ya kustaajabisha sana. Imepiga maendele makubwa kiuchumi, ingawa wananchi wengi, haswa vijijini, bado maskini. Pia, ni nchi ambayo haina Amani ya kudumu, kila siku wanapigana 《Tigray vs Oromo》.Ukija kwenye hali ya hewa ndio usiseme. Ukame kila mara. Internat yao ni ya kuunganisha na gundi, akini uchumi wao unaendele kukua.
Upande mwingine, Ethiopia Wana Diaspora kubwa sana, haswa kule US (takribani Ethiopians 400, 000 wanaishi huko) Pengine hii inasaidia kwenye remittance inayorudishwa, Sina uhakika. Maana Hawa jamaa ni ma- entrepreneurs by nature. Kila walipo lazima wafungue biashara.