Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Bunge la Tanzania ni baraza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotunga sheria na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Majukumu ya Bunge yametamkwa katika Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Nchi, kwa maneno yafuatayo:
“Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano, ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya Wananchi, ya kusimamia na kuishauri Serikali ya Muungano pamoja na vyombo vyake vyote katika utekelezaji
wa majukumu yake “
Hivyo basi Bunge ni Chombo cha Uwakilishi wa Wananchi. Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge
linaweza:-
1. Kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya Umma.
2. Kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa Bajeti.
3. Kujadili na kuridhia Mpango wowote wa muda mrefu au muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa Mpango huo.
4. Kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo Sheria.
5. Kujadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambayo kwa masharti yake
inahitaji kulidhiwa
Kazi ya bunge sio kusifia wala kuunga mkono mambo. Mbunge ni mwakilishi wawananchi.
Mbunge Msukuma amekuwa akijitahidi sana kusimama katika majukumu ambayo mbunge anatakiwa kuyafanya. Pia kuna yule mbunge wa Kahama wanajitahidi sana.
Kama mbunge hawezi kuwahoji mawaziri anakua anakiuka katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63 (2). Wabunge tuamke wananchi hawana huwezo wa kuhoji mpaka watembelewe na viongozi.
Mmechaguliwa kuhoji hoji. Kuuliza sio ujinga. Na ukijibiwa kama umeridhika na majibu tulia. Kama hujaridhika hoji tena. Hiyo ndio kazi yako kikatiba.