Ni mbunge Mpina pekee anayetumia ubunge wake ipasavyo, wabunge mliobaki naomba tujikumbushe majukumu ya Bunge la Tanzania

Umemaliza mkuu Meneja
 
Mpina Luhaga aongee tu, ila Bunge hili si la wananchi ni la CCM au Bunge linalowawakilisha mapolisi.
 
Kujadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambayo kwa masharti yake
inahitaji kulidhiwa
Mikataba inawndikwa kwa kiingereza tena cha kisheria, wabunge wanaokijua hawazidi 50 na wanaweza kununuliwa the rest wagonga meza
 
Hakuna Wabunge mle kuna Wajumbe wa HALMASHAURI KUU CHAMA kwenye Jengo la BUNGE
 
KWa Tanzania ya sasa watu wanaofanya mambo sahihi ndio tunawaona hawapo sahihi; nakubaliana na wewe kabisa kwamba ndugu Mpina anafanya kazi sahihi ambayo ndio HASA kazi za mbunge but kwa mazoea yetu ya sasa tunamshangaa kwasababu yupo tofauti na wenzie; sikuelewa hata mantiki ya Msukuma kumdhalilisha Luhaga Mpina kwa jambo lile.
Police au hakimu anae kataa rushwa kwasasa jamii inamshangaa, kwamba huyu vipi? Ndio kinacho tokea kwa Luhaga Mpina. Sitashangaa bwana Mpina akipigwa chini kwenye KURA za maoni mwaka 2025, siwezi kushangaa
 
Nepotism ndo inatusumbua Tanzania,kama baba yake alisema sasa hivi wanalamba asali,Samia ataweza kumwondoa kweli?

Nilishangaa sana Baba yake kuongea kihuni vile. Tunalamba asali, Tunalamba asali, tunalamba asali mpaka 2030.

Mtoto absolutely incompetent yeye ni visingizio na kulamba asali.

They are both are out of touch with interests of common people and reality.
 
Fisiemu haijawahi kumpenda mtetea wanyonge mtu anayesimamia haki. Akiendelea hivi yakiomkuta ndugai yatamkuta ana luhaga mpina.
Mark my words
 

Wanaweza kumpiga chini hata kumtafutia zengwe, kumchafua. Lakini katika jamii ya Watanzania tunahitaji watu wachache kujitolea, kutimiza wajibu wao / kazi zao bila woga au kujali sana maslahi binafsi nini kitawatokea.

Tukiwa na wabunge hata nusu, robo wanaotimiza wajibu wao. Watanzania wengi watapata nafuu ya maisha, changamoto nyingi zitatatuliwa haraka na rasilimali za nchi kutumika kwa manufaa ya taifa.
 
Fisiemu haijawahi kumpenda mtetea wanyonge mtu anayesimamia haki. Akiendelea hivi yakiomkuta ndugai yatamkuta ana luhaga mpina.
Mark my words

Hivi hawa wanaosema ukweli, wanaowapigania Wananchi, maslahi ya umma kwanini wasianzishe group lao, chama chao,
ambacho kitakuwa kinapigania haki, maslahi mapana ya Watanzania.

Wapo wakutosha lakini naona bado hawana ujasiri wa kujitokeza, kuungana na kulipigania taifa wazi wazi. Nina uhakika wakijitokeza kwa idadi ya kutosha wataungwa mkono na Watanzania wengi.

Why do they allowed themselves to be ignored, ostracized, marginalised and sidelined?
 
Infwakiti wabongo midomoni tupo vizuri mnoo ila vitendo sifuri matumbo njaaa. Asikwambie mtu kelele za kina mpina ni kwa sababu wamenyinwa ugali waliokuwa wanautafuna enzi za jiwe. Lait wakipewa tonge na mchuzi wanakaa kimya. Mzee wa shule SLOW SLOW alikuwa anapang'ang'a sana sasa kimyaaaaaaaaa. Dont mess up with the FISIEMU. Jamaa wana system ya kunyamazishe vidomo domo.
 

Wapo waliosimamia maslahi ya Taifa bila uoga kama Augustino Mrema 1995 upigaji, rushwa, ufisadi kila mtu kula kwa urefu kamba zake, mfumuko wa bei, uhuni ulipokithiri

Japo hakutangazwa mshindi, lakini ilisaidia kidogo serikali iliyokuja kupunguza upigaji, rushwa, kwamba kila kitu ni rukhsa.

Awamu iliyofuata japo kwa kiwango fulani na ilijaribu kuunda taasisi imara kusimamia rasilimali za nchi na maslahi ya Watanzania wengi.

His effort was not in vain, kuna mabadiliko ya msingi yalitokea kutokana na jitihada, juhudi na harakati zake. Tunahitaji wakina Mrema wapya wa kizazi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…