Ni Mchezaji gani wa Taifa Stars alikuvutia kwenye mchezo wao na Algeria jana?

Ni Mchezaji gani wa Taifa Stars alikuvutia kwenye mchezo wao na Algeria jana?

Taja huo mtandao, tuujue, mana mitandao yenye kuheshimika wamempa Novatus
Kuna hatari unapotumia takwimu za computer au kura za watu pekee

Ona huu mtandao umetoa top ratings hizi kwa kutumia kura za watu zaidi ya 13,000

Kwa upande wa Algeria
WhatsApp Image 2023-09-08 at 15.12.34.jpeg

Top ratings kwa upande wa Tanzania

WhatsApp Image 2023-09-08 at 15.12.35.jpeg
 
Hizo ziko computer generated au wakati mwingine zinaweza kuwa biased na wapigaji kura wenyewe. Na kama kigezo ni rating nimekuonyesha hiyo hiyo FOTMOB wameonyesha wachezaji 3 wana rating sawa na Novatus.

View attachment 2743205
View attachment 2743206
Sawa, ila hawawez kuwa 4 POTM, hivyo kitendo cha kumchagua Novatus lazima kuna vigezo wamecheki, na huwez nambia mitandao yote wakosee, haya tuassume hatuwaamin Fotmob, nambie nani tumuamini?
Leta hio website unayosema mchezaji mwenye rating ndogo zaidi wa Algeria ana rating kubwa kuliko mchezaji mwenye rating kubwa ya Tz
 
Kuna hatari unapotumia takwimu za computer au kura za watu pekee

Ona huu mtandao umetoa top ratings hizi kwa kutumia kura za watu zaidi ya 13,000

Kwa upande wa Algeria
View attachment 2743216

Top ratings kwa upande wa Tanzania

View attachment 2743217
Yan mzee unataka unambie ile kazi zilizofanywa mle ndani ndio rating ya 3? Au 4 hizo za wa Algeria? Huo mtandao haupo serious, No wonder haufahamiki
 
Yan mzee unataka unambie ile kazi zilizofanywa mle ndani ndio rating ya 3? Au 4 hizo za wa Algeria? Huo mtandao haupo serious, No wonder haufahamiki
Hao nadhani rating ya juu zaidi mchezaji anaweza kupewa ni 5, hawaendi hadi 10.

Fanya hivi, kama unatumia simu google "Tanzania va Algeria" halafu yakija matokeo ya jana hapo juu nenda bonyeza "Player ratings". Najaribu kuangalia kama ni google wanakusanya kutoka vyanzo mbalimbali na kupata wastani au inabase kwenye kura zinazopigwa na google pekee.

Ninachotaka kusema ni kuwa njia zote mbili ukizitumia za computer au za kura bila kufanya analysis unaweza usipate majibu sahihi. Ndiyo maana huyo mchambuzi alipotoa hiyo taarifa wengi wameikosoa.
 
Jana mchezaji mmoja tu wa Tanzania kacheza kuliko wote na ndiye ametuvusha hatuwa hii:

Mama Samia ndiye aliyeucheza mpira wa jana. Kacheza peke yake, tumpe mauwa yake.

Sio Mtume tena? Astagafilullah
 
Joseph kaniki Golotha
Said mwamba kizota
Shadrack Nsajigwa fuso
Juma Nyosso

Hawa wapewe maua yao[emoji95][emoji95][emoji95]
 
Fotmob wamempa Novatus man of the match, sofascore pia, AI score pia, kwa hio nadhani alikuwa sahihi
Pia huo mtandao wa AiScore umewapa wachezaji 4 wa Algeria rating kubwa kumzidi Novatus, sasa atakuwaje man of the match?

Sawa, ila hawawez kuwa 4 POTM, hivyo kitendo cha kumchagua Novatus lazima kuna vigezo wamecheki, na huwez nambia mitandao yote wakosee, haya tuassume hatuwaamin Fotmob, nambie nani tumuamini?
Leta hio website unayosema mchezaji mwenye rating ndogo zaidi wa Algeria ana rating kubwa kuliko mchezaji mwenye rating kubwa ya Tz
Screen Shot 2023-09-08 at 4.29.33 PM.png

Halafu hii mitandao na wewe usiiamini sana, ona picha walizotumia. Kwenye picha ya Mzamiru wamemuweka Boko, ya Mzize wamemuweka Kibu, ya Mwamnyeto wamemuweka Djuma Shabani

Na hao sofascore pia wamewapa Novatus na Tougani tie ya 7.4. Kwa hiyo naanza kudhani una nia ya kupotosha watu kama mwenzio

Screen Shot 2023-09-08 at 4.47.22 PM.png
 
Feisal hajawahi kufanya maajabu kimataifa iwe taifa staz, yanga na sasa azam hata hasipokuwepo hakuna pengo lolote. Kuhusu samata katubeba sana kipindi ambacho umri wake ulikua unaruhusu tatizo pro alikua peke yake ila kwa sasa umri ushamtupa mkono akiwa taifa staz lazima acheze kwa tahadhari kuepuka majeruhi ili kulinda kibarua chake ulaya. Hata angekua Cristiano Ronaldo asingeweza kutufikisha mbali peke yake kwaiyo Samata tumpe heshima yake.
Heshima ya mbwana ally samatta tunampa na maua yake tunamkabidhi. ila pamoja na kwamba ni mchezaji mzuri kiwango chake binafsi hakiniridhishi,
 
Mimi ni Utopolo ila nilimkubali sana Kibu Denis, alijituma na kukaba kuliko wachezaji Wote!
 
Jana mchezaji mmoja tu wa Tanzania kacheza kuliko wote na ndiye ametuvusha hatuwa hii:

Mama Samia ndiye aliyeucheza mpira wa jana. Kacheza peke yake, tumpe mauwa yake.
Kachezea wapi? Mambo mengine ni kumtusi mkidhani mnamsifia
 
Jana mchezaji mmoja tu wa Tanzania kacheza kuliko wote na ndiye ametuvusha hatuwa hii:

Mama Samia ndiye aliyeucheza mpira wa jana. Kacheza peke yake, tumpe mauwa yake.
Naona wanasiasa wanalazimisha kutumia mafanikio ya soccer kupata umarufu.
 
Back
Top Bottom