Ni mdudu yupi kati ya hawa unamuogopa zaidi?

Ni mdudu yupi kati ya hawa unamuogopa zaidi?

Aisee kunguni washenzi wanaweza kukuzalilisha hadharani, kuna nyumba nihwawahi kaa niliipanga na furniture zake nilizozikuta kumbe ina wanajeshi(kunguni). Unaweza ukatoka zako vizur na nguo zako ghafla anatokeza kwenye shati upo na watu wa maana. Alafu hawaishi kirahisi labda uhame kwa muda upige dawa ya maana.
Kuna nyumba nilihamia kumbe kuna hao viumbe,na nilikua siwajui nlikua nadhani ni vimende vidogo dogo 😂😂😂,
Aiseee ponea yangu nilihama nyumba na vitu nikavipiga fumigation,yaani nawaogopa hao viumbe hata kuwataja tu nahisi kama watatokea 😩
 
Kuna siku nimeua mende mbele ya Mwanamke mmoja alipomuona yule mende wallah alitetemeka mpaka akashindwa kula chakula....nilicheka sana
 
Kama mwanaume kuogopa wadudu ni udhaifu wa aina yake.

Ila kuna hawa viumbe!
Ni vijidudu vidogo sana ila viliwahi kunishusha kwenye mti moja kwa moja mpaka chini!

Heri ufikie jiwe kwa kuanguka juu ya mti kuliko mashambulizi ya hawa wadudu

7ce26117cefad4640919fea92b5786e8.jpg
 
Kuna mji ama eneo pale moshi pana itwa chekereni!
Kumbe ilikua ni maana yake hio , halafu kweli reli imekatika pale.
hata chuga kuna chekereni, kuna wazungu walikuwaga na mashamba maeneo hayo, sasa wakati wanawatuma wafanyakazi ambapo wangekatiza reli wakawa wanawaambia check train, check train, waja wakawa wanasema chekereni ndo likawa jina rasmi.
 
Kuna dudu Fulani lenya mdomo mbaya na surabaya waichilamu Huwa wanalila kinaitwa ngamia? Nashindwa kuelewa unaacha kula mnyamba Handsome kama kitimoto unakula ngamia kweli linavyotisha?
 
Kuna nyumba nilihamia kumbe kuna hao viumbe,na nilikua siwajui nlikua nadhani ni vimende vidogo dogo 😂😂😂,
Aiseee ponea yangu nilihama nyumba na vitu nikavipiga fumigation,yaani nawaogopa hao viumbe hata kuwataja tu nahisi kama watatokea 😩
Aah, kudadeki nilikua siwajui pia ila mziki wao niliucheza usiku hulali😂😂
 
Unawafahamu nzuki au nyuki?
hao wadudu wanakukalisha chap kwa haraka!
Niliwahi pigwa tukio na nyuki ..ata baada ya kupona haikuniacha sawa kisaikolojia sometime ata Inzi wakining’onga nazua taharuki 😂
 
Tandu wamejaa sana Dar es salaam na Pwani. Kiboko yao ni rungu.

Nge ni nadra sana kuonekana, ila huyo mwamba aki kung'ata utahadithia.
 
Back
Top Bottom