Ni mdudu yupi kati ya hawa unamuogopa zaidi?

Kuna nyumba nilihamia kumbe kuna hao viumbe,na nilikua siwajui nlikua nadhani ni vimende vidogo dogo 😂😂😂,
Aiseee ponea yangu nilihama nyumba na vitu nikavipiga fumigation,yaani nawaogopa hao viumbe hata kuwataja tu nahisi kama watatokea 😩
 
Kuna siku nimeua mende mbele ya Mwanamke mmoja alipomuona yule mende wallah alitetemeka mpaka akashindwa kula chakula....nilicheka sana
 
Kama mwanaume kuogopa wadudu ni udhaifu wa aina yake.

Ila kuna hawa viumbe!
Ni vijidudu vidogo sana ila viliwahi kunishusha kwenye mti moja kwa moja mpaka chini!

Heri ufikie jiwe kwa kuanguka juu ya mti kuliko mashambulizi ya hawa wadudu

 
Kuna mji ama eneo pale moshi pana itwa chekereni!
Kumbe ilikua ni maana yake hio , halafu kweli reli imekatika pale.
hata chuga kuna chekereni, kuna wazungu walikuwaga na mashamba maeneo hayo, sasa wakati wanawatuma wafanyakazi ambapo wangekatiza reli wakawa wanawaambia check train, check train, waja wakawa wanasema chekereni ndo likawa jina rasmi.
 
Kuna dudu Fulani lenya mdomo mbaya na surabaya waichilamu Huwa wanalila kinaitwa ngamia? Nashindwa kuelewa unaacha kula mnyamba Handsome kama kitimoto unakula ngamia kweli linavyotisha?
 
Aah, kudadeki nilikua siwajui pia ila mziki wao niliucheza usiku hulali😂😂
 
Unawafahamu nzuki au nyuki?
hao wadudu wanakukalisha chap kwa haraka!
Niliwahi pigwa tukio na nyuki ..ata baada ya kupona haikuniacha sawa kisaikolojia sometime ata Inzi wakining’onga nazua taharuki 😂
 
Tandu wamejaa sana Dar es salaam na Pwani. Kiboko yao ni rungu.

Nge ni nadra sana kuonekana, ila huyo mwamba aki kung'ata utahadithia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…