Ni meseji gani unayotumiwa kwenye simu ila hupendi?

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Habari wakuu,

Binafsi kila nikipokea muamala, muda si mrefu unaingia ujumbe wa mtandao husika wa kunitaka nicheze kamari. utaona ghafla '' Ndugu mwenye namba 0713 xxxxxx, ushaandaliwa TZS 800,000,000 jaribu leo. Na jumbe nyingi mfano wa hizi.

Je, ni ujumbe gani hauupendi kabisa utumiwe kwenye simu yako?
 
Ile pesa tuma...jina litakuja...

Mganga mashuhuri anatibu....

Chanjo ya corona.....

Umepokea tsh...kwa maelezo zaidi piga...(message inatumwa na namba ya tigo,halafu kwa maelezo ya kupiga wameweka namba ya voda au airtel)
 
Ndugu Mteja, katika kusheherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja, tunakushukuru kwa kuichagua Tigo. Tunafurahi kuendelea kukuhudumia.Heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja
 
Mimi meseji za Vodacom na Halotel ndiyo zimefanya hadi niblock notifications kwenye app ya messages. Na kwa bahati nzuri si mtumiaji sana wa meseji za kawaida.
 
DSTV SC ********* inakata -. Piga *150*53# kulipia 145,000. Kwa huduma ya extra view lipia TZS27,000. Pakua Showmax kupitia www.showmax.com 🥲
 
Kuashiria bando linaisha
 
Deni la M-pawa,ile kuorodheshwa kwenye wadaiwa sugu,sijui nitakosa sifa kukopesheka na taasisi za kifedha!!!!?

Kuna kipindi walinipigia kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…