Ni meseji gani unayotumiwa kwenye simu ila hupendi?

Ni meseji gani unayotumiwa kwenye simu ila hupendi?

TSH 500,000 TASLIM au sehemu ya Tsh 10,000,000 LEO zipo mikononi mwako! Jiunge na SOKA sasa uweze kukamata mkwanja huu PAPO HAPO tuma neno SOKA kwenda 15670!
 
VodaCom na meseji zao za
"Umeishiwa salio au umesitisha"
Zile meseji ni kero kama nzige vile
 
Kuna muda unasubiri jumbe ya maana, unaacha shughuli zako kuangalia simu, mara wiki ya huduma kwa wateja ,benki ulishasahau
 
Hawakusumbui na sms uchwara za kutishia kukufungia?

Sms isiyo na mashiko kwa ujumla zinaniboa, nambie, my, jibu swali uwe milionea, za teenagers ( hapa unatamani awe mbuzi umnywe supu tu) fambastic!
Wataifunga kabisa muda si mrefu. Utakuwa huna uwezo wa kuunga kifurushi chochote, kuweka vocha kwa njia yoyote, kupokea msg, kuangalia salio nk.

Ukitumiwa pesa itaingia lakini hutapata msg, hiyo pesa hutaweza kuifanya chochote labda umwambie aliyetuma airudishe.
Yaani hata menu ya tigopesa hutaweza kuingia.

Kwa kifupi access za huduma zote za mtandao na nje ya mtandao mfano menu ya bank, ving'amuzi, menu za kubeti zitakufa kikamilifu.
Utakachoweza kwenye hiyo laini yako ni kupokea simu tuu.

SAMAHANI
Huu ujumbe nilikuwa namjibu Faana aliyesema haweki vocha mwezi wa 9 huu, bahati mbaya nime-quote kwako.
 
Haina neno kaka, nilishamuelekeza mtu ili wasinifungie
 
Mpendwa 767xxxxxx, wiki inakaribia kuisha..
Umeangalia kama WEWE ndio MSHINDI wa droo ya Tsh.Mil100, Tsh.Mil10 au Tsh.Mil1?
Angalia ZAWADI papo hapo na uingie kwenye droo ya leo!
Unaweza KUSHINDA Tsh.Mil100 PAPOHAPO!
Piga*150*00#>3>6
MESSAGE YA VODA TOKA NAMBA 15544 HIVI KUNA ALISHAWAHI SHINDA?
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Hongera kwa kuichagua tigooo 😜😜😜

Ndugu Mteja, katika kusheherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja, tunakushukuru kwa kuichagua Tigo. Tunafurahi kuendelea kukuhudumia.Heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja
 
Wanakuhofia Mkuu 🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️🏃🏽‍♂️

Mbona hizi msg mimi sipati? Au wameniruka?
 
Back
Top Bottom