NI MIAKA SASA HATUPO NAYE

NI MIAKA SASA HATUPO NAYE

Mwanzo nilidhani nilidhani ni uturi( wat wa pwani hasa wanawake huwa wanatumia kujifukiza ili wanukie mwili na ngu zao) , Siku moja kuna rafiki yangu alikuja nayo nyumbani kwetu akaniambia onja mimi nilichukua kidogo sana nitia mdomoni nikameza , Nilitapika sana na nilisikia kizungu zungu kutwa nzima siku ile.

Ila nilipata uelewa kuwa sio kila kitu cha kuonja na kwa mtindo ule ndio vijana wengi hua mwanzo wa kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa na mihadarati mingine kwa kufuata ushawishi wa marafiki.
 
Kuna jamaa tulikuwa tunasoma naye, siku moja akaja home na hiyo kitu. Nikajifanya mnaa, nikabwia nyingi.

Karibia nife aisee. Dunia ilikuwa inazunguka kwa kasi halafu kibaya zaidi tulikuwa juu ghorofani, wenyewe tulikuwa tunapaita summit. Ile siku siwezi kusahau.

Huyu jamaa yangu mara ya mwisho kumuona ilikuwa karibu na Wizara ya Elimu pale magogoni, alishakuwa chizi. Sijui kama alipona.
 
Hahaha. .hiyo kuber ilikuwa ni matata. .binafsi sijawahi kuitumia aise. .mimi na vilevi tuko against sana
Hii nliwahi kuijaribu kipindi na miaka 15, siku hio nlipoteza fahamu kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Ile nazinduka nikawahi fasta kwenda kuvaa nguo za shule najua nshachelewa darasani (Bi mkubwa akaniuliza vipi leo umewehuka). Ni balaaa
 
Hahaha
Hii kitu kuna mate wangu saivi mkuu Wa mkoa alitumia baada ya kuvutiwa na mates wengine wahindi walivokuwa wanazitumia tukiwa skuli, jamaa aliachia haja kubwa live bila chenga....jamaa alijifanya mwamba akaibugia yote kwa pupa kuonyesha alivo kidume.
Mheshimiwa RC nakusabahi kutoka namanyere hapa!
Noma sana hii ngoma
 
Back
Top Bottom