Nimedika Mikoa yote Na Wilaya Zote za Tanzania Bara.
Visiwani nimefika Unguja tu, Pemba Sijafika.
Nnachoweza kwambia maisha yakikupiga kabisa kijana timkia kati ya Ngara, Kibondo au Kasulu. Kamata eneo, panda mihogo, Subiri kuiuza Rwanda na Congo.
Kwa sasa Tanzania bara tupo connected sawa sawia na mtandao wa barabara za rami, maeneo ambayo zamani usingependa ambiwa nenda sasa unaweza kwenda bila shida yoyote, yani ukiniamsha usiku unaniambia tuitafute Bumbuta-Kondoa, Tunduru-Ruvuma, Kipili-Namanyere-Sumbawanga, Karema-Tanganyika, Mgeta Nchombe hadi Mlimba TX, Matombo-Kisaki hadi Mvuha, hata Kahunda-Buchosa, kote huko tutaenda bila shida, ila kipande cha kuitafuta Loliondo tokea Ngorongoro ndio ntawaza mara mbilimbili na kukagua gari sawa sawa.