Ni mikoa mingapi umewahi kufika na una maoni gani Kwa ujumla ujumla baada ya kupita huko

Ni mikoa mingapi umewahi kufika na una maoni gani Kwa ujumla ujumla baada ya kupita huko

jiji la Mwanza Kwa mapana ni dogo kama ilivyodhaniwa Hasa ukilinganisha na dsm.

ukiamka asubuhi hata kutumia daladala unaweza kuzunguka kila kona hadi kufikia saa saba ukalimaliza
Dar inaonekana kubwa kwa vile wilaya hadi wilaya hakuna mapori... kwa maana ya eneo Dar ni ndogo..
 
Tabora, Kigoma, Kagera, Morogoro, Arusha , Moshi, Mara, Tanga Dom, Iringa, Dsm na sasa Mwanza.

Nilichoona ni kwamba kuna gap kubwa kati ya wenye nacho na wasionacho, masikini ni wengi sana.

Lakini pia ukikosa pesa jilaumu mwenyewe usiseme Tz watu hawana pesa bali sema mimi sina pesa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesafiri mikoa yote tanzania isipokuwa rukwa na pemba tu.

Mikoa yoote ukitoa majiji nadhan inafanana tu kimaisha... Ubaya uliopo kwa mikoa mingi ni kutoendelea kwa maeneo ya vijijini...

Ukifika dodoma town pazuuri... Ukizama bush utajuta...


Ila top 5 mikoa bora kwangu ukiondoa dsm ni.

Mwanza.
Dodoma.
Mbeya.
Arusha.
Mtwara.


Ya kipimbi.
Singida.
Kigoma.
Lindi.
Ruvuma.
Na mikoa mipya yoote.
Pwani.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijatembea sana TZ ila nimefanikiwa kuishi mikoa 8 tofauti mingi kanda ya pwani, kaskazini na kati.

Dodoma palinishangaza maana niliwasili humo kipindi cha masika palikua green kweli kweli ila ilipofikia kipindi cha kiangazi ilibaki miti tu isiyokuwa na majani huku ardhi nayo ikiwa haina uoto wowote.

Mkoa wa Kilimanjaro nilishangaa sana kusikia watu wakisema "Naenda Moshi" hapo labda anatokea Dar lakini hata Moshi hafiki kwao ni Same au anapita Moshi kwao ni Hai. Niakaja kugundua watu wengi hudhani mkoa wote wa Kilimanjaro huitwa Moshi kumbe Moshi ni wilaya tu (Moshi Mjini na Moshi Vijijini).

Morogoro kusema kweli ni mkoa pekee ambao niliishi nikiwa sielewi, jiografia ya kichwa ilivurugika maana nilikua naishi Kihimbwa Road kule Forest juu lakini siku zote niliona jua likichomoza kutoka Magharibi na kuzama Mashariki. 😂😂

Ahaa yaani ww ulikua jirani..kihimbwa road..asbh baridii
 
Nimedika Mikoa yote Na Wilaya Zote za Tanzania Bara.
Visiwani nimefika Unguja tu, Pemba Sijafika.

Nnachoweza kwambia maisha yakikupiga kabisa kijana timkia kati ya Ngara, Kibondo au Kasulu. Kamata eneo, panda mihogo, Subiri kuiuza Rwanda na Congo.

Kwa sasa Tanzania bara tupo connected sawa sawia na mtandao wa barabara za rami, maeneo ambayo zamani usingependa ambiwa nenda sasa unaweza kwenda bila shida yoyote, yani ukiniamsha usiku unaniambia tuitafute Bumbuta-Kondoa, Tunduru-Ruvuma, Kipili-Namanyere-Sumbawanga, Karema-Tanganyika, Mgeta Nchombe hadi Mlimba TX, Matombo-Kisaki hadi Mvuha, hata Kahunda-Buchosa, kote huko tutaenda bila shida, ila kipande cha kuitafuta Loliondo tokea Ngorongoro ndio ntawaza mara mbilimbili na kukagua gari sawa sawa.
 
Nimezunguka Tanzania bara yote, top 5 ya mikoa bora niliyoiona ukitoa Majiji

1. Geita, watu wanapiga hela kwenye madini sio mchezo

2. Songwe, uwepo wa boda ya Tunduma

3. Morogoro, hii wanaitaga njia panda ya ulaya pia kilimo chochote kinakubali

4. Shinyanga, uwepo wa migodi kama buzwagi na buli inayopatikana mji wa kahama, ambapo hela ipo nje nje

5. Ruvuma, hasa Songea panafa sana kwa kilimo
 
Nimesafiri mikoa mingi katika mikoa ilionishangaza ni Dodoma, Tanga, Singida
Dodoma kuna jangwa na upepo mkali mno nakumbuka first day kweny huu mkoa msosi wangu uliingia vumbi kwa mama ntilie aise nilimaindi fursa hamna kabisaa. Tanga ni mkoa ambao nilijiuliza kuishi kwao Handeni ni wavivu hawana mifugo hawalimi wanalia njaa wakati ardhi ipo na inavutia, radio station inayoshika ni Abood tuu simu haipandishi mnara mtandao wowote niliishi pale kama msukule ata nchi ikipinduliwa nisingejua maana ata lowasa walikuwa wanajua yupo ccm bado ingali kashaamia chadema, singida wanawake wanajirahisisha mno hasa kwa wageni. Mikoa nilioipenda ukitoa DSM ni, Geita,Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mtwara


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom