Ni mikoa mingapi umewahi kufika na una maoni gani Kwa ujumla ujumla baada ya kupita huko

Ni mikoa mingapi umewahi kufika na una maoni gani Kwa ujumla ujumla baada ya kupita huko

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
watz tunasimangwa Kwa kutotembea nje ya nchi. Naamini humu Tutakuwa tumebobea Ktk kutembea ndani ya nchi.
binafsi nimeishi na nimetembea mikoa 14 tz Bara na Mmoja Zanzibar.

nilichojifunza
Ni DSM tu ambapo watu huwahi kuamka asubuhi, wanatembea chapchap, watu wazima hawataki shkamoo.
 
Nimetembea mikoa 24 tanzania Bara. Ukiondoa kigoma na Tanga. Lakini nilichokiona ni umaskini uliyokithiri katika jamij zetu. Majority ya watu hawana furaha na maisha maana uhakika wa kesho hauko mikononi mwao.
Wengi Hawana uwezo wa uhakika wa chakula kwa siku za mbele ikitokea dharura yoyote ile. Kama huna uwezo wa kutunza chakula kwa siku 10 zijazo hali ni mbaya sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
watz tunasimangwa Kwa kutotembea nje ya nchi. Naamini humu Tutakuwa tumebobea Ktk kutembea ndani ya nchi.


binafsi nimeishi na nimetembea mikoa 14 tz Bara na Mmoja Zanzibar.

nilichojifunza
Ni dsm tu ambapo watu huwahi kuamka asubuhi, wanatembea chap chap, watu wazima hawataki shkamoo.
Sijafika Zanzibar na Kigoma pekee katika nchi hii... Nilichoona ni kuwa mikoa karibu yote iliyopitiwa na Waarabu ipo nyuma kimaendeleo... UMWINYI MWINGI...
 
jiji la Mwanza Kwa mapana ni dogo kama ilivyodhaniwa Hasa ukilinganisha na dsm.

ukiamka asubuhi hata kutumia daladala unaweza kuzunguka kila kona hadi kufikia saa saba ukalimaliza
 
Sijatembea sana TZ ila nimefanikiwa kuishi mikoa 8 tofauti mingi kanda ya pwani, kaskazini na kati.

Dodoma palinishangaza maana niliwasili humo kipindi cha masika palikua green kweli kweli ila ilipofikia kipindi cha kiangazi ilibaki miti tu isiyokuwa na majani huku ardhi nayo ikiwa haina uoto wowote.

Mkoa wa Kilimanjaro nilishangaa sana kusikia watu wakisema "Naenda Moshi" hapo labda anatokea Dar lakini hata Moshi hafiki kwao ni Same au anapita Moshi kwao ni Hai. Niakaja kugundua watu wengi hudhani mkoa wote wa Kilimanjaro huitwa Moshi kumbe Moshi ni wilaya tu (Moshi Mjini na Moshi Vijijini).

Morogoro kusema kweli ni mkoa pekee ambao niliishi nikiwa sielewi, jiografia ya kichwa ilivurugika maana nilikua naishi Kihimbwa Road kule Forest juu lakini siku zote niliona jua likichomoza kutoka Magharibi na kuzama Mashariki. 😂😂
 
Sijaenda Ruvuma,katavi,rukwa,mtwara ,kagera,lindi na pemba
Tarime is the best . Ukipiga yowe tu majirani washafika na silaha kusaidia.
Sehemu zingine watakuja kukupa pole asubuhi uliishaumizwa
nyamongo kule watu wote wanaafya. ni kijiji pekee chenye wanavijiji wenye magari na msouth za kutosha.

pia wanaupendo usio na urafiki
 
Cjafika kigoma na bukoba kwingine bara na visiwan nimekanyaga,kila sehem na tabia zao labda ulenge nikupe Story za mkoa upi haswaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania ni kubwa sana aisee..nilishangaa wakati naenda kusini eti njia nzima hoteli ni moja tu..Star com pale Nangurukuru..ukitoka hapo unapiga pori la maana kuitafuta Lindi..yaani nitofauti na mikoa mingine njiani kumechangamka.Mtwara sio kubaya sana...hata hivyo bado ni mikoa inayofunguka taratibu..
 
Nimebakiza mikoa ya Mtwara, Lindi Pemba na Mara tu, Umasikini upo katika mikoa yote tena kwa viwango vinavyolingana. Kipimo kinachotumika kulinganisha kiwango cha umasikini kwa kiasi kikubwa ni ujenzi wa nyumba za tofari na kuezeka nyumba kwa mabati, kitu ambacho ni kawaida katika mikoa yote.
 
Nimefika Bukoba, Mwanza,Dar,Mara,Moro,Arusha,Shinyanga ni hiyo tu.

Mwanza ni jiji la miamba kweli sema umoja(nzengo) nilijifunza.

Dar fursa kibao na jiji linalobadilika kila uchao sema joto kali.

Bukoba wajuaji sana lakini wameshindwa jenga mji wao, pia roho mbaya

Arusha kwanza baridi kali kwa mjini lakini baadhi ya wilaya zake joto kali kama upo jangwani

Moro watu wanalima kweli, sema bei ya vitu vyake pale mjini ni ghali sana kama nguo n.k

Mara ni mkoa wa watu wa kazi sema hofu ni kuibiana mifugo.
 
Back
Top Bottom