SoC03 Ni Mimi na Wewe

SoC03 Ni Mimi na Wewe

Stories of Change - 2023 Competition

Abdul Hoza

Member
Joined
Dec 4, 2022
Posts
7
Reaction score
6
Ni mimi na Wewe
Ili kujenga jamii bora yenye kuzingatia maadili na desturi za kiafrika basi watekelezaji wakubwa ni mimi na wewe. Mimi na Wewe ndio tunaoweza kuibadilisha jamii au kubadilisha jamii zetu na ziwe katika mstari mnyoofu na wenye kuleta matunda kuanzia sasa na vizazi vingine vijavyo. Jamii zetu kwa sasa zimekubwa na janga la mmomonyoko wa maadili kuanzia kundi la watoto hadi kundi la wakubwa na hali hii imekuwa ikileta matokeo hasi kwenye jamii sasa je nani ambaye atabadilisha haya basi sio wengine ila ni MIMI NA WEWE.

Ni Mimi na Wewe.
Ili taifa lolote liweze kuendelea kunahitajika uwepo wa nguvu kazi mbalimbali kulingana na uwabikaji wa makundi mbalimbali yaliyopo katika taifa husika. Nguvu kazi kubwa inayohitajika katika taifa huwa ni vijana, vijana ni kundi ambalo huamua kesho ya taifa itakuwaje hasa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na taifa kwa ujumla. Vijana tuamke, vijana tushikamane, vijana tulioneshe taifa nini nguvu yetu na umuhimu wetu kwa ujumla. Ni mimi na Wewe.

Ni Mimi na Wewe.
Hivi sasa nafasi nyingi za uongozi hasa katika mataifa mengi ya ulaya zipo chini ya uongozi wa vijana hasa kuanzia umri 30 mpaka 40. Lakini ukija kwetu sisi ni tofauti, vijana bado hatujaaminiwa kuwa katika nafasi kubwa za uongozi na huwa tunaonekana kama nafasi hizo ni viatu vikubwa kwetu,je nani wa kulizungumza hili basi sio wengine bali ni MIMI NA WEWE. Vijana tuamke na kulizungumzia hili kwa maslahi mapana ya taifa letu. Sisi ndo wenye kesho na keshokutwa yetu,kizazi chetu kinategemea kikutwe makubwa kutoka kwetu,tuliongee na kulipigania hili.

NI MIMI NA WEWE.
Niite Kijana.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom