Azam wasipo kuwa makini, basi naona Boss wa Info amejipanga kuwa piku akishirikiana na kampuni moja kutoka Mauritius - Mr.Mfuruki kichwa sana yule atakuja kubadiri soko hili beyond expectations za Wateja.
Tatizo la Azam TV si wabunifu, ni kweli wana vifaa vingi vya kisasa na studio nzuri - beyond that wanaendeleza mambo kama mashirika ya UMMA ya wacha liende - watu wabunifu wangepata facilities kama zile specifically studios wangezifanyia wonders! Siwasemi vibaya lakini tuwe wakweli hapa ubunifu hawana kabisa, nguvu zao zote zinaelekezwa zaidi kwenye masuala ya mipira ya hapa na Ulaya, sio kwamba nataka kuwaribia biashara - Nina uzoefu wa muda mrefu wa masuala haya nimeishi kwa nchi za wenzetu kwa miaka mingi sio kwamba nasema mambo ya kubuni tu, wanapaswa kujirekebisha.
Nakuunga mkono, Azam ubunifu ni ZERO. Mfano, upande wa michezo, wawe wanawatembelea wachezaji na kuonyesha wanaishi vipi, mbwana samata wamfuate huko kuonyesha anavyoishi na changamoto anazozipata huko ili na wachezaji huku wahamasike, wamfuate hata Ngassa south, yaani wawe wanafuata matukio na wanaofanya hayo matukio.
Upande wa soka wamchukue Shaffih Dauda, naona jamaa ni mbinifu ktk vipindi vya soka.
Pia wafunguke kidogo na kutambua kuwa soko kubwa ni vijana, wawe na vipindi vya vijana vingi bila kusahau vya wazee na watoto.
Muvi waonyeshe latest za kibongo ktk sinema zetu sio unaweka muvi ya 2005 alafu unarudia kila baada ya wiki hiyo hiyo!
Pia wawe na session ya muvi zile za waswazi yaani zilizotafsiriwa na yule muongea kiswahili ili Azam iwe burudani kwa wote kweli, mshiko wanao, waandae TZ GOT TALENT, shoo iliyoenda shule, achana na vile viupuuzi vya BSS, wahakikishe wanakava kila angle.
Entertainment, wamchukue Salama Jabir, ana mawazo sana ya ubunifu vipindi vya vijana.
Hata wawe na kipindi cha kuzunguka zunguka kama Siz Kitaa cha Clouds lakini hiki kiwe ktk vikao vile vya kahawa mida ya jioni, wawe wanaenda kwa wazee na hao vijana kahawani na kujadili mada fulani, wazee na vijana wanaokutanaga hapo huwa na topic motomoto zenye kukava kila angle na wazee hutoa maneno ya busara kama ujumbe kwa vijana! Huwa ni fun sana. Sio mbaya kila wiki wanawatembelea na wasanii kama wale wa comedi kina Joti na kuongea nao yale mautani yao unprepared, yaani sio yale mambo ya TAKE 1, TAKE 2, hapana! Ni unaongea nae utani na anaendelea kupngea utani na pumba zake kwenye TAKE moja tu! Kipindi kinakuwa more genuine!