Ni mkakati gani Azam tv umetumia kuteka soko?

Ni mkakati gani Azam tv umetumia kuteka soko?

Safari zangu mikoani nimeshangaa wingi wa madishi ya Azam tv kila ni endepo. Siyo siri tena Azam tv imeteka soko la tv ya malipo. Je ni mbinu ipi Azam umetumia kuteka soko hadi kuwaungusha dstv zuku na kadhalika?
Mkuu ni ligi kuu tu hakuna kingine!! Leo hii DSTV akichukua haki za kuonyesha ligi kuu Azam chalii
 
Azam wasipo kuwa makini, basi naona Boss wa Info amejipanga kuwa piku akishirikiana na kampuni moja kutoka Mauritius - Mr.Mfuruki kichwa sana yule atakuja kubadiri soko hili beyond expectations za Wateja.

Tatizo la Azam TV si wabunifu, ni kweli wana vifaa vingi vya kisasa na studio nzuri - beyond that wanaendeleza mambo kama mashirika ya UMMA ya wacha liende - watu wabunifu wangepata facilities kama zile specifically studios wangezifanyia wonders! Siwasemi vibaya lakini tuwe wakweli hapa ubunifu hawana kabisa, nguvu zao zote zinaelekezwa zaidi kwenye masuala ya mipira ya hapa na Ulaya, sio kwamba nataka kuwaribia biashara - Nina uzoefu wa muda mrefu wa masuala haya nimeishi kwa nchi za wenzetu kwa miaka mingi sio kwamba nasema mambo ya kubuni tu, wanapaswa kujirekebisha.
mkuu naona mada imekupita kushoto, mada inasema kwanini azam tv wameteka soka, wewe unasema azam tv sio wabunifu. Tuambie kwanza kwa nini wameteka soko?
 
mm nimeshangaa kitu chengine kidogo tuu. azam fc wana likes 310,000 wakati timu zite 15 zilizibaki ukijumlisha likes zao hazifikii hapo. hii ni facebook.
 
Katika ulimwengu wa biashara kuna kitu kinaitwa Branding na kilichowafanya hivyo azam tv ni brand yao mama kwa maana ya Azam,Kwanza brand ni muonekano na ahadi unayoiweka kwa wateja wako, sasa basi kutokana na hilo kuna brand ambazo hutengeneza sub-brand na kuziacha zijitegemee na zingine huzibeba sub-brand ziitegemee brand mama mfano Coca ndio mmiliki wa Sprite, Fanta.. lakini brand zote zinajitegemea hauwezi kukuta kitu cha Fanta kinachanganya na coca katika kujitangaza au kuwafikia wateja) na mfano wa brand kubeba sub-brand ni kama ( Castle inaibeba Castle lager.)

Sasa basi Azam inabeba sub-brand zake nyingi, Azam Mango, Azam juice, Azam Andazi n.k,kutokana na hilo hivyo sub-brand hutumia jina na nafasi ya brand mama kupata nafasi katika soko haya nilitaka kwanza mjue hilo nakuja kujibu swali sasa.

Azam Tv wamefanikiwa kutokana na kwanza kutumia jina ka Brand mama ambayo imesambaa katika sekta nyingi, vyakula,vinywaji,n.k hivyo imekuwa rahisi kuaminika,pili imelisoma soko la visimbuzi linakosa nini na watu wanapenda nini,tatu mbinu za kujitangaza na kiwango cha kutimiza lengo la wateja wao.

hivyo ndivyo vilivyoipandisha Azam Tv katika soko la visimbuzi.
 
Azam wasipo kuwa makini, basi naona Boss wa Info amejipanga kuwa piku akishirikiana na kampuni moja kutoka Mauritius - Mr.Mfuruki kichwa sana yule atakuja kubadiri soko hili beyond expectations za Wateja.

Tatizo la Azam TV si wabunifu, ni kweli wana vifaa vingi vya kisasa na studio nzuri - beyond that wanaendeleza mambo kama mashirika ya UMMA ya wacha liende - watu wabunifu wangepata facilities kama zile specifically studios wangezifanyia wonders! Siwasemi vibaya lakini tuwe wakweli hapa ubunifu hawana kabisa, nguvu zao zote zinaelekezwa zaidi kwenye masuala ya mipira ya hapa na Ulaya, sio kwamba nataka kuwaribia biashara - Nina uzoefu wa muda mrefu wa masuala haya nimeishi kwa nchi za wenzetu kwa miaka mingi sio kwamba nasema mambo ya kubuni tu, wanapaswa kujirekebisha.
Nakuunga mkono, Azam ubunifu ni ZERO. Mfano, upande wa michezo, wawe wanawatembelea wachezaji na kuonyesha wanaishi vipi, mbwana samata wamfuate huko kuonyesha anavyoishi na changamoto anazozipata huko ili na wachezaji huku wahamasike, wamfuate hata Ngassa south, yaani wawe wanafuata matukio na wanaofanya hayo matukio.
Upande wa soka wamchukue Shaffih Dauda, naona jamaa ni mbinifu ktk vipindi vya soka.
Pia wafunguke kidogo na kutambua kuwa soko kubwa ni vijana, wawe na vipindi vya vijana vingi bila kusahau vya wazee na watoto.
Muvi waonyeshe latest za kibongo ktk sinema zetu sio unaweka muvi ya 2005 alafu unarudia kila baada ya wiki hiyo hiyo!
Pia wawe na session ya muvi zile za waswazi yaani zilizotafsiriwa na yule muongea kiswahili ili Azam iwe burudani kwa wote kweli, mshiko wanao, waandae TZ GOT TALENT, shoo iliyoenda shule, achana na vile viupuuzi vya BSS, wahakikishe wanakava kila angle.
Entertainment, wamchukue Salama Jabir, ana mawazo sana ya ubunifu vipindi vya vijana.
Hata wawe na kipindi cha kuzunguka zunguka kama Siz Kitaa cha Clouds lakini hiki kiwe ktk vikao vile vya kahawa mida ya jioni, wawe wanaenda kwa wazee na hao vijana kahawani na kujadili mada fulani, wazee na vijana wanaokutanaga hapo huwa na topic motomoto zenye kukava kila angle na wazee hutoa maneno ya busara kama ujumbe kwa vijana! Huwa ni fun sana. Sio mbaya kila wiki wanawatembelea na wasanii kama wale wa comedi kina Joti na kuongea nao yale mautani yao unprepared, yaani sio yale mambo ya TAKE 1, TAKE 2, hapana! Ni unaongea nae utani na anaendelea kupngea utani na pumba zake kwenye TAKE moja tu! Kipindi kinakuwa more genuine!
 
mkuu naona mada imekupita kushoto, mada inasema kwanini azam tv wameteka soka, wewe unasema azam tv sio wabunifu. Tuambie kwanza kwa nini wameteka soko?

Mimi nilikuwa na sababu zangu kutumbukiza nilicho kisema, wao kama wao wamenielewa - sasa wewe kama uliona nilicho zungumza ni irrelevant the best you could've done no ku move on kama wasomaji wengine.

Haya mambo ya ku dwell katika Ku insult intelligence za binadamu wenzako speaks volume about u'r persona.
 
Nakuunga mkono, Azam ubunifu ni ZERO. Mfano, upande wa michezo, wawe wanawatembelea wachezaji na kuonyesha wanaishi vipi, mbwana samata wamfuate huko kuonyesha anavyoishi na changamoto anazozipata huko ili na wachezaji huku wahamasike, wamfuate hata Ngassa south, yaani wawe wanafuata matukio na wanaofanya hayo matukio.
Upande wa soka wamchukue Shaffih Dauda, naona jamaa ni mbinifu ktk vipindi vya soka.
Pia wafunguke kidogo na kutambua kuwa soko kubwa ni vijana, wawe na vipindi vya vijana vingi bila kusahau vya wazee na watoto.
Muvi waonyeshe latest za kibongo ktk sinema zetu sio unaweka muvi ya 2005 alafu unarudia kila baada ya wiki hiyo hiyo!
Pia wawe na session ya muvi zile za waswazi yaani zilizotafsiriwa na yule muongea kiswahili ili Azam iwe burudani kwa wote kweli, mshiko wanao, waandae TZ GOT TALENT, shoo iliyoenda shule, achana na vile viupuuzi vya BSS, wahakikishe wanakava kila angle.
Entertainment, wamchukue Salama Jabir, ana mawazo sana ya ubunifu vipindi vya vijana.
HAYA MAWAZO INABIDI WAYALIPIE MKUU
 
Wakati Azam anaingia kwenye soko la TV ya kulipia alimkuta Startimes kashaanza kuota mizizi(Naiondoa DSTV sababu watu wengi hawawezi kumudu hasa vijijini) lakini tatizo la Star times alikuwa akitumia antenna hivyo maeneo mengi kusumbua hasa huko mikoani ulikotembelea na maeneo mengine ikuwa haipatikani kabisa akaja kupata akili kashaachwa mataa.

Nakumbuka wakati wanaanza watu wanauliza mkoa fulani mmefika, wanajibu simple, Tanzania nzima. DSTV imepitwa sababu ya gharama plus kuna kundi kubwa lina nguvu sana ya kuamua nyumbani waangalie nini ambalo DSTV walishindwa kuliona, nao ni mama, watoto wake na wafanyakazi wa ndani. Watu hawa hawako interested sana na mipira na content ya kiingereza. Wao michezo ya Kiswahili, kina Joti na vipindi vingine vya Kiswahili wakaacha mataa hapo.

Kingine kama mdau alivyoeleza, brand yake ina mbeba, nakumbuka walichelewa kuanza kulingana na matarajio mpaka ikabidi mipira irushwe TBC wakati wanakamilisha. Watu walikuwa hawaishi kuuliza mnaanza lini bila kujua kilichomo simply kwa sababu wamekariri brand ya Azam haibahatishi.
 
Back
Top Bottom