Ni mke wa mtu, ni mzuri, ANANITAKA nifanyeje?

ni wakumuogopa kama ukoma huyo mke wa mtu,ashume angekuwa ni mkeo ndo anajilengesha kwa mtu

Mke wake yeye akijilengesha kwa mtu, huyo mtu lazima atamla!....So be fair, nayeye amtafune tu huyu wa sasa hivi. Kwanini aidhulumu nafsi yake!? Kwanza hata hapa kaja kujishaua tu, lakini akilini mwake anajua kwamba hana hata nia ya kutomla huyo dada!
 

pamoja na sifa zote za uzuri lakini kwa haraka naona kama huyo dada (1) si muaminifu - ameshajieleza mumewe anasafirisafiri ili ushawishike haraka kuwa hata ukiwa nae haina probleme - muogope mtu huyo mke wa mtu halafu anajitongozesha mwenyewe kwa mwanamume. (2) ana tamaa - anatamani maisha mazuri ambayo pengine mumewe hajayamudu, kinachomvutia zaidi kwako ni hilo gari ulilonalo!
ushauri wangu: pamoja na uzuri wake, lakini usiingie kwenye majaribu ya kuwa nae kwa kuwa anataka kukung'ang'ania kwa kuwa ana kitu anafaidi kwako mfano huo usafiri lakini siamini km ana mapenzi ya kweli achana nae, pia wewe una mchumba, huyo dada atakupotezea muda kwa kuwa nae kimapenzi na mchumba akijua mkiachana utakuja kugundua kuwa huwezi kumuoa huyo mke wa mtu badala yake utakosa mwana na maji ya moto! aidha siku mume wake akikugundua... ndio utajua bamia haitengenezi juisi... kwa ufupi utajiharibia mambo mengi sana kwa uhusiano wako huo.
 
kaka mwepuke kama ukoma, ukimwendekeza utajikuta umeharibu kwa mchumba. Wanaume hatuna ujasiri wa kukaa karibu na hawa watu kwa karibu tusichombeze, hasa kama ushamzimia. Dawa ni kukimbia fasta mpaka ajue unamkimbia. Amen
 
Ndio maana waume wengine yuko radhi atembee kwa miguu kama mkewe kaharibikiwa na gari
lakini ampa mkewe, wanajua mambo ya lifti hizi loooooooo
 
Mweleze mchumba wako hiki kisa halafu umuombe ushauri... Ni yeye pekee atakupa ushauri wa kukufaa..
 
"....Anaishi na mume wake na wana mototo mmoja......" Mkuu kumbuka BIG DOG POSE washasema mke wa mtu ni Sumu a.k.a HATARI.
 
Wajameni,
Huyu ndie alietuaga humu kwamba ameachiwa mke na mume au...?


 
Du kumbe ni issue ya July 2011, jamaa kesharudi na anamchuma mkali atajakubonda na ki-mkoko chako sasa kaangalie mchumba wako mwaka huu nae hana mtu? kaa karibu nae asijegeuka hawa na HAWA
 
Hahahahah. . . .
Sie. . . labda kama amekuja na ID nyingine.

Maana nimekuwa natafuta thread ya huyu muagaji angalau inayokaribia na masuala ya mke wa mtu. Lakini nimeipata hii tu nikadhani ni yeye ila kaja kivingine!
 
Maana nimekuwa natafuta thread ya huyu muagaji angalau inayokaribia na masuala ya mke wa mtu. Lakini nimeipata hii tu nikadhani ni yeye ila kaja kivingine!

Yenyewe iko hapo chini, ina kichwa kinachosema kwaherini.
 

sikuelewi ujue! Private car inasimama kituoni kufanya nini?
 
Kuna mwenzako mmoja yeye kwa sasa anaaga watu baada ya kutembea na mke wa mtu, yaliyomkuta anayajua mwenyewe.Kila la kheri.
 
Huo ni Udhaifu wa kuonyesha unaendekeza libeneke kaka na hauko matured enough to resist vishindo vya kina dada. inakuwa kama kale kamnyama pori kakiona kichaka tu M*Vi yanambana. Dont think like a Man, Think Like a Real Man (Gentleman) Reject her with wisdom instead ya kumkimbia kumpa lift. Be honest you have a girl and you love her!! she will respect you and admire you even more. and kama ni mwanamke mstaarabu atakuwa best wako kwa mtindo mwingine na sio kwa hayo unayoyadondoshea udenda!!
Sorry to say But hivi ndio maana tunakufa ovyo kwa kutokuwa waaminifu kwa wapenzi wetu na kuweka mbele tamaa.
Good Luck
 
Kaka ikimbie zinaa!Acha kumpa lift.Akikutafuta mwambie unapitia sehemu.Asubuhi wahi kidogo kupndoka.One wiki tu ajakuelewa then ataachana na wewe.Anakueleza mume wake ni mtu wa kusafiri ili kukupa nafasi ya kumtumia eeh.Kaa chonjo!Vipimo vya ngoma siku hizi havionyeshi kama ni positive au negative!oh
 
Mke wa mtu ni sumu usijaribu kuchombeza yatakuja yakukute huo ndio ushauri wangu kwako.
 
Kuna mwenzako mmoja yeye kwa sasa anaaga watu baada ya kutembea na mke wa mtu, yaliyomkuta anayajua mwenyewe.Kila la kheri.

Huwezi jua labda hawa ni mtu yule yule. Sisi tunafanya masihara kumbe mwezetu yamemfika!
 

Mkuu nimependa ushauri wako umejaa hekima sana pia naheshim ushauri wa wadau wengine pia.Naungana na wewe kumshauri hivo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…