Ni mke wa mtu, ni mzuri, ANANITAKA nifanyeje?

Dogo, watakudokta ulimboka. Mke wa mtu si tu sumu bali ni DDTii. Kwanza huoni kashakuwa screpa! je jamaa akikuachia kimoja si itabidi utunze na kusomesha watoto wa mwanamme mwenzio.
 
Wewe na hamu za wake za watu ziache kwa ushauri story hizi zimo humu kibao endelea kuperuzi utapata majibu mengi sana tushatoa
 
Mtoa mada,kulikoni story nzito kama hii ukaishusha usiku wa manane? Au ulikuwa naye pembeni?
Mshawahi kufanya romance bila ku go all the way?
Ningekuwa wewe kusema ukweli ningempa dozi kisha niingie mitini,utaache mdondo bana?

Kama kawaida yako banana man!
 
Dogo kuna mambo yanayowezekana na wewe unaonekana kumpenda mke wamtu,kuwa makini sana,kama unaweza kuiba iba ila kwa kujiachia kwako futi sita yaja.
 


Huo ndio msingi wa kuungangania na la pili ni kukata mahusiano na huyo mwanamke kwani Mola amesema; Hawi watatu kati ya mwanamke na mwanamme, zaidi ya shetani. Ubaya zaidi nikuwa shetani anakuwa kiungo mzuri anaewafahamu udhaifu wenu.
 
Tatatizo analiendeleza yeye mwenyewe, kama vipi amlambe, au aoe na amtambulishe mke wake aone kama atajileta tena...

Huu ndio ushauri mzuri kabisaa!! Atafute mke wake mwenyewe, 30years kama noma na iwe noma OA mkuu.
 
Nakushauri mkuu umaanishe unachokisema, ikibidi hata mawasiliano na huyo mwanamke punguza ibakie salamu inatosha. Inavyoonekana mna wakati mwingi wa kukaa peke yenu faragha mpaka anakueleza matatizo yake na kukuomba ushauri. Kka ikimbie dhambi kwa miguu yako miwili wala sio kwa kutambaa.

Kama huamini wanawake waliokengeuka imani hutumiwa na ibilisi soma vitabu vitakatifu utamkuta Hawa(Alidanganywa na nyoka akala tunda), Delila(Alitumiwa na wafilisti kumuua Samson), Mke wa Ayubu(Aliyemshauri mume amkufuru Mungu), Sara wa Ibrahimu (Aliyemshauri mumewe amtwae kijakazi), Potifa mke wa Mfalme(Aliyemtaka Yusuph kwa nguvu).

Je nawewe unataka uingie kwenye historia hii?
 
Je waweza kuweka moto kifuani na nguo zako zisiungue?kata mawasiliano naye ibaki salamu tu .Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa huyo hujiangamiza mwenyewe
 
Piga mzigo huo kwa maufundi ya hali ya juu. Hizi bahati haziji mara mbili.
 
NA wewe usiwe DHAIFU achana nae ni suala la maamuzi tu..ukijishauri hapa inaonekana na wewe ni DHAIFU...chukua hatua mamlaka unaayo yatumie...
 
usiruhusu ukaribu na yeye tena kama kweli hutaki kama unatamani utajiju but you are going to pay for that,so be prepared
 
Utashughulikwa na wewe ndugu! Kimbia kabisa!
 
Hii ni sawa na kumbusu mamba shavuni.....usichukue ushauri huu.
Mzee umenifurahisha sana na hii kitu...."Kumbusu mamba shavuni" ......teh, teh,teh. wewe ungemwaacha angie kichwa kichwa ili aoteshwe kitenisi.
 
Mtoa mada,kulikoni story nzito kama hii ukaishusha usiku wa manane? Au ulikuwa naye pembeni?
Mshawahi kufanya romance bila ku go all the way?
Ningekuwa wewe kusema ukweli ningempa dozi kisha niingie mitini,utaache mdondo bana?

Acha kuganganya. labda kama anatafuta support hapa. lakini anajua ukweli.
 
Kila mla cha mwenzie na chake pia huliwa.

Kabla ya kutembea na mke wa mtu unatakiwa ujiulize hivi kama na wewe mke wako ukagundua anatembea nje ndoa unajisikiaje, kama jibu utaona ni poa hata mke wako akichukuliwa na mtu basi na wewe endelea na hiyo program ya kuchukua mke wa watu. Otherwise mke wa mtu ni sumu ndugu yangu kama alivyochangia Rogie
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…