Ni Mkenya au Mtanzania, yupi anayeweza kutupa maana ya methali hii?

Cha mkufuu mwanafuu Hali,na akila hufa....Cha mwanafuu mkufuu hula na akila hafi..
 
Cha mkufunzi mwanafunzi huwa hali, na akikula atakufa. Lakini cha mwanafunzi mkufunzi aweza hula na akikula hawezi kufa.
 
Hapo naona kuna watu wawili... Mkufuu na Mwanafuu!!

Mmoja akila cha mwenzake, poa tu (akila "ha") lakini yule aliyeliwa chake nae akita ale cha aliyemla, inageuka kuwa nongwa ("hu")!

Anyway, hiyo ni literal meaning!

Hakika Kiswahili kigumu!!
Upo sahihi mkuu, Mwalimu hula cha mwanafunzi na hadhuriki na mwanafunzi akila cha mwalimu inakuwa shida
 
Wapi kiima na kiarufu kwenye hiyo sentensi?
 
Hii hata mimi nimetoka kapa, ila nahisi hapo mkufuu ruksa kula cha mwanafuu.....
Mokaze na Bishop Hiluka ndio wamepata jibu sahihi. Maana yake ni kuwa jambo ambalo mkufunzi anaweza kufanya mwanafunzi hawezi na akijaribu atashindwa. Jambo ambalo mwanafunzi anaweza kuifanya mkufunzi anaweza kuifanya na akijaribu atafaulu. Yaani jambo ambalo Tanzania inaweza kufanya Kenya pia inaweza kufanya na jambo ambalo Kenya inaweza kufanya Tanzania haiwezi kufanya na ikijaribu itashindwa.





Full meaning yake bila kuifupisha ni hivi:

Cha mkufunzi mwanafunzi hali na akila hufa. Cha mwanafunzi mkufunzi hula na akila hafi
 
wasalimie hapo kibera
 

Yeah iliwahi kujadiliwa huku Methali Tata
 
Mtoa mada bado hujapata jibu? Watu wametililika hapo.
 
Hii sio methali bwana
 
Siku hizi ni vice versa. Mkufunzi anashindwa na mwanafunzi. Wanafunzi wamemea pembe hatari hadi mkufunzi anaogopa kuzikata! 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…