Ni mkoa gani umeshawahi kufika na hautamani kurudi tena?

Bukoba , mji mdogo naoupenda zaidi Tz. Pametulia, beach life, vyakula vya asili, hakuna uswahili
 
Nimefika Lindi,Mtwara,Morogoro, Dodoma,Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Mwanza na kote naweza kurudi anytime labda kwasababu huwa naenda kimatembezi na kukaa siku 3-5 tu.
Tanzania ni nchi nzuri.
Tunatofautiana namna kuyaona mambo tu.

Kuna mdau anasema Singida hakufai but ukienda kwa jicho la mtalii...Singida kuna miinuko na mawe inayovutia kutazama...kuna ziwa Singida upande wa mashariki kuna mawe yanotoa view nzuri sana.

Kigoma kuna beach tamu sana.

Tatizo la wengi ni jicho la kuona vitu vipya hawana, umasikini hupofusha macho.
 
Singida ipo kwenye mipango yangu.
 
Kwa mikoa niliyofika ,mbeya,moro,kigoma,tanga ,mwanza ,mara, shinyanga, na arusha kote huko nilipapenda ingawa kwa arusha ni changamoto nilizopata sisahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…