Ni msanii gani wa Kenya anakubalika sana Tanzania?

Ni msanii gani wa Kenya anakubalika sana Tanzania?

Na hapo ndipo siwaelewi. Hebu nifafanulie
Sikiliza nyanyangu, katika nchi zetu changa kama hizi ambazo watu bado tunajaribu kupambana na ukabila, kitu chochote kile kinachoeleza au kutofautisha watu kutokana na ukabila lake, ni hatari sana kukiendekeza, hata kama lengo ni zuri, lakini madhara yake huwa hayarekebishiki.

Mambo kama matumizi ya lugha za makabila katika Government offices, matumizi ya mavazi ya makabila au ya kidini katika Government offices, kuruhusu redio au magazeti kutumia lugha au ishara za kabila, yote haya ni hatari sana.
 
Sasa unataka kusema tupige marufuku nyimbo zinazoimbwa kwa lugha za kikabila? Naelewa Tanzania yote mnazungumza kiswahili na nyimbo zote zinaimbwa kwa hii lugha. Je,hizo kabila za kichagga,kisukuma,na spinach zipo kweli ama ni majina tu?
Mtanzania Saida Karoli alikuwa anaimba nadhani ni kwa kihaya, na nyimbo zake zilisikizwa sana. Nandani kuna nyimbo moja ambayo Diamond ametumia line zake za kihaya. Ile ya chambua kama karanga. Waache unafik.
 
Unanikosha sana Mkuu. Nilienda Nairobi kwa mara ya kwanza, nikipofika mahali panaitwa Athi River kwenye njia inayoelekea Mombasa jamaa akaweka hizo nyimbo mpaka tulipofika stand ya magari ya Riverside......!

Tangu siku hiyo nilizipenda hizo nyimbo, jamaa alikuwa anaitwa Mwangi na contacts zake ninazo.

Baadae nikampata GF anatokea Muthaiga....ananipenda sana hadi leo na anajua napenda hizo nyimbo so nikawa nikiweka miadi naye lazima aniandalie hizo nyimbo.

Aaaah! [emoji15][emoji15][emoji15] Haya basi, kuuulaaa ngoma! Kwa raha zako! [emoji1]
 
Nazungumza kuhusu ninachokijua, ni ngumu sana kumkuta Mtanzania anaskliza wimbo wowote nje ya Bongo flava, hili nimeliona sana kwenu na hiyo nchi yenu nimeitembea zaidi ya wengi wenu humu, nimekatiza mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya hivyo napafahamu vizuri sana.
Yaan ukute Mtanzania amekaa anaskliza wimbo usio Bongo flava, utatembea sana, ni wachache labda waliobahatika kutoka na kuishi nje ya nchi na kurudi, ila wengine wote mumefungiwa ndani ya zizi moja, athari za ujamaa hizo, inalemaza mtu kiakili kwamba hauwezi kuwaza nje ya ulichoelekezwa.
Leo hii Bongo flava imeanza kubadilika na kuiga mitindo ya Kinijeria na ndio maana unakuta wengine wenu mumeanza kuwakubali hao Wanaijeria.
Lie of the day.

We Ulikuwa unainteract na watu gani mkuu ?
Mbona rahisi sana kukuta wabongo wanaskiza Nyimbo za mataifa na mitindo kibao?
 
Unanikosha sana Mkuu. Nilienda Nairobi kwa mara ya kwanza, nikipofika mahali panaitwa Athi River kwenye njia inayoelekea Mombasa jamaa akaweka hizo nyimbo mpaka tulipofika stand ya magari ya Riverside......!

Tangu siku hiyo nilizipenda hizo nyimbo, jamaa alikuwa anaitwa Mwangi na contacts zake ninazo.

Baadae nikampata GF anatokea Muthaiga....ananipenda sana hadi leo na anajua napenda hizo nyimbo so nikawa nikiweka miadi naye lazima aniandalie hizo nyimbo.
Hahaha! [emoji1]
Safi sana. Nilidhani ni utani jombaa. Mziki ni 'universal' na sio lazima usikie lugha inayotumiwa ili upende mziki wenyewe. Kuna mtindo fulani wa kuvutia kwenye nyimbo za kiasili, ndio maana hata Saida Karoli nilimkubali sana enzi zile. Kuna nyimbo flani hivi ya msaani fulani wa Bongo, ya zamani kidogo, inaitwa lugha gongana pale mwisho mwisho ametumia kilugha kuwaamkua watu wa kwao, freshi sana. Hivyo ni vitu ambavyo huwa tu kwenye nyimbo za lugha za kiasili.
 
Poapoa mkuu. Hiyo lugha gongana aliimba Noorah.
Hahaha! [emoji1]
Safi sana. Nilidhani ni utani jombaa. Mziki ni 'universal' na sio lazima usikie lugha inayotumiwa ili upende mziki wenyewe. Kuna mtindo fulani wa kuvutiwa kwenye nyimbo za kiasili, ndio maana hata Saida Karoli nilimkubali sana enzi zile. Kuna nyimbo flani hivi ya msaani fulani wa Bongo ya zamani kidogo inaitwa lugha gongana pale mwisho mwisho ametumia kilugha kuwaamkua watu wa kwao, freshi sana. Hivyo ni vitu ambavyo huwa tu kwenye nyimbo za lugha za kiasili.
 
Back
Top Bottom