Ni msanii gani wa Kenya anakubalika sana Tanzania?

Na hapo ndipo siwaelewi. Hebu nifafanulie
Sikiliza nyanyangu, katika nchi zetu changa kama hizi ambazo watu bado tunajaribu kupambana na ukabila, kitu chochote kile kinachoeleza au kutofautisha watu kutokana na ukabila lake, ni hatari sana kukiendekeza, hata kama lengo ni zuri, lakini madhara yake huwa hayarekebishiki.

Mambo kama matumizi ya lugha za makabila katika Government offices, matumizi ya mavazi ya makabila au ya kidini katika Government offices, kuruhusu redio au magazeti kutumia lugha au ishara za kabila, yote haya ni hatari sana.
 
Sasa unataka kusema tupige marufuku nyimbo zinazoimbwa kwa lugha za kikabila? Naelewa Tanzania yote mnazungumza kiswahili na nyimbo zote zinaimbwa kwa hii lugha. Je,hizo kabila za kichagga,kisukuma,na spinach zipo kweli ama ni majina tu?
Mtanzania Saida Karoli alikuwa anaimba nadhani ni kwa kihaya, na nyimbo zake zilisikizwa sana. Nandani kuna nyimbo moja ambayo Diamond ametumia line zake za kihaya. Ile ya chambua kama karanga. Waache unafik.
 
Unanikosha sana Mkuu. Nilienda Nairobi kwa mara ya kwanza, nikipofika mahali panaitwa Athi River kwenye njia inayoelekea Mombasa jamaa akaweka hizo nyimbo mpaka tulipofika stand ya magari ya Riverside......!

Tangu siku hiyo nilizipenda hizo nyimbo, jamaa alikuwa anaitwa Mwangi na contacts zake ninazo.

Baadae nikampata GF anatokea Muthaiga....ananipenda sana hadi leo na anajua napenda hizo nyimbo so nikawa nikiweka miadi naye lazima aniandalie hizo nyimbo.

Aaaah! [emoji15][emoji15][emoji15] Haya basi, kuuulaaa ngoma! Kwa raha zako! [emoji1]
 
Lie of the day.

We Ulikuwa unainteract na watu gani mkuu ?
Mbona rahisi sana kukuta wabongo wanaskiza Nyimbo za mataifa na mitindo kibao?
 
Hahaha! [emoji1]
Safi sana. Nilidhani ni utani jombaa. Mziki ni 'universal' na sio lazima usikie lugha inayotumiwa ili upende mziki wenyewe. Kuna mtindo fulani wa kuvutia kwenye nyimbo za kiasili, ndio maana hata Saida Karoli nilimkubali sana enzi zile. Kuna nyimbo flani hivi ya msaani fulani wa Bongo, ya zamani kidogo, inaitwa lugha gongana pale mwisho mwisho ametumia kilugha kuwaamkua watu wa kwao, freshi sana. Hivyo ni vitu ambavyo huwa tu kwenye nyimbo za lugha za kiasili.
 
Poapoa mkuu. Hiyo lugha gongana aliimba Noorah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…