~**~ Ni Msemo wa Kikwetu ~**~

~**~ Ni Msemo wa Kikwetu ~**~

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Mapenzi ni kama ndoto, twaota ikatokea,
Hata kuwe viroboto, kitandani yatokea,
Iwe baridi na joto, na jasho kudondokea,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu!!

Mapenzi ni kama homa, yanahitaji tabibu,
Moyo wako wasimama, hadi aje wa muhibu,
Ni dawa iliyo njema, tangu enzi za mababu,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu!!

Mapenzi ni kama chai, yanahitaji sukari,
Kinywa chapata uhai, ukaondoa munkari,
Ukaivalia tai, si chungu kama shubiri,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama chelezo, yataka pa kuelea,
Yakakupa kitulizo, pale unapoelea,
Upepo uje kwa kizo, wajua kuogelea,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama ndoana, uitupe kwa makini,
Wawili mje shikana, kwa amana na imani,
Kwa penzi liloivana, lililojaa moyoni,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama jabari, juu yake wasimama,
Kukuepusha hatari, likaulinda mtima,
Penzi liko akhuyari, kwa wababa na wamama,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama upepo, huvuma unakopenda,
Yakakukumba ulipo, ukaacha randaranda,
Yakakupatia pepo, moyoni ukayafunda,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama asali, ukauchonga mzinga,
Ukitaka kukabili, nyuki hawatakuzinga,
Penzi si kitu muhali, wewe usije jivunga,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Mapenzi kama shairi, yenye lugha yenye kina,
Ndiyo hayo ya bukhari, ni mapenzi yalo nona,
Yafaa yako nadhari, waziwazi nimenena,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Mwanakijiji karibu, Jukwaa mahusiano,
Upate yetu mahabu, Siasa ni migongano,
Watakuvuta sharubu, Raha upate mswano,
Jukwaa mahusiano, Hapa ni kwako nyumbani.

Siasa ni kitu gani, Kichwa wajiumizia,
Mapenzi ni yako fani, Hakika umebobea,
Njoo tupe burudani, na hekima yako pia,
Mapenzi mahusiano, Jukwaa lakuhitaji
 
mwanakijiji karibu, jukwaa mahusiano,
upate yetu mahabu, siasa ni migongano,
watakuvuta sharubu, raha upate mswano,
jukwaa mahusiano, hapa ni kwako nyumbani.

Siasa ni kitu gani, kichwa wajiumizia,
mapenzi ni yako fani, hakika umebobea,
njoo tupe burudani, na hekima yako pia,
mapenzi mahusiano, jukwaa lakuhitaji

that is my msacha.....:d
 
Chrispin unataka nihamishe na jembe kabisa.. maana yawezekana kwenye siasa kuna ukame kwa kweli.. hakuna mazao yanayoota huko!!
 
,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

mkuu hiki kiitikio kwangu kina kigugumizi. hata kama hujapenda ila ukipendwa nawe upende? hapa tunahitaji double coincidence of want ili mapenzi yatokee. vinginevyo ni mitafaruku tu kama hii tunayoona enzi hizi kutokana na hako kamsemo
 
,

Mapenzi kama upepo, huvuma unakopenda,
Yakakukumba ulipo, ukaacha randaranda,
Yakakupatia pepo, moyoni ukayafunda,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

watu mna taaluma nyingi ...vipaji hivyo
hongera mwanakijiji nimelipenda shairi lote lakini sana nimependa beti hiyo
 
mkuu hiki kiitikio kwangu kina kigugumizi. hata kama hujapenda ila ukipendwa nawe upende? hapa tunahitaji double coincidence of want ili mapenzi yatokee. vinginevyo ni mitafaruku tu kama hii tunayoona enzi hizi kutokana na hako kamsemo

Maneno mazito haya, je una experience unayoweza kushare?
 
mkuu hiki kiitikio kwangu kina kigugumizi. hata kama hujapenda ila ukipendwa nawe upende? hapa tunahitaji double coincidence of want ili mapenzi yatokee. vinginevyo ni mitafaruku tu kama hii tunayoona enzi hizi kutokana na hako kamsemo

Kingi huwa nasikia mara nyingi sana watu walioumizwa wakitumia hiyo lugha ya kina MMK ntapenda atakayenipenda, and I end up asking myself the same question....

kwamba hata kama hujamdondokea basi vile kakupenda umkubali and then what?? you learn to love the person coz he loves you??
 
watu mna taaluma nyingi ...vipaji hivyo
hongera mwanakijiji nimelipenda shairi lote lakini sana nimependa beti hiyo

FL1.. inaonekana na wewe yamekukumba eh!? ndiyo hivyo lakini penda unapopendwa.. wanasema utakuja penda usipopendwa.. ndiyo yanakuwa mateso hapo.
 
mkuu hiki kiitikio kwangu kina kigugumizi. hata kama hujapenda ila ukipendwa nawe upende? hapa tunahitaji double coincidence of want ili mapenzi yatokee. vinginevyo ni mitafaruku tu kama hii tunayoona enzi hizi kutokana na hako kamsemo

maana yake ni kuwa usipende mahali ambapo hupendwi.. kwa maneno mengine "pendaneni"!!!
 
maana yake ni kuwa usipende mahali ambapo hupendwi.. kwa maneno mengine "pendaneni"!!![/QUOTE]

OOOH!!!
MMK umenikumbusha na wimbo wa kanaisani sasa
...nawapa amri mpya mpendane, asema Bwana kama vile mimi nilivyowapenda ninyi....(God knows version yangu ya huo wimbo nilivokuwa mtoto LOL!!)
 
Kingi huwa nasikia mara nyingi sana watu walioumizwa wakitumia hiyo lugha ya kina MMK ntapenda atakayenipenda, and I end up asking myself the same question....

kwamba hata kama hujamdondokea basi vile kakupenda umkubali and then what?? you learn to love the person coz he loves you??
i think love is not learned but experienced naturally. hizo ni dalili za kutapatapa ila zinaweza kusaidia baadae, kwamba utampenda anaekupenda. ila mara nyingi tatizo hujirudia tena, and suicide may be a poor solution
 
Mwanakijiji na Bibi yetu huwa unamwagia mashairi matamu kama hayo?
 
Back
Top Bottom