Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mapenzi ni kama ndoto, twaota ikatokea,
Hata kuwe viroboto, kitandani yatokea,
Iwe baridi na joto, na jasho kudondokea,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu!!
Mapenzi ni kama homa, yanahitaji tabibu,
Moyo wako wasimama, hadi aje wa muhibu,
Ni dawa iliyo njema, tangu enzi za mababu,

Mapenzi ni kama chai, yanahitaji sukari,
Kinywa chapata uhai, ukaondoa munkari,
Ukaivalia tai, si chungu kama shubiri,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu.
Mapenzi kama chelezo, yataka pa kuelea,
Yakakupa kitulizo, pale unapoelea,
Upepo uje kwa kizo, wajua kuogelea,

Mapenzi kama ndoana, uitupe kwa makini,
Wawili mje shikana, kwa amana na imani,
Kwa penzi liloivana, lililojaa moyoni,

Mapenzi kama jabari, juu yake wasimama,
Kukuepusha hatari, likaulinda mtima,
Penzi liko akhuyari, kwa wababa na wamama,

Mapenzi kama upepo, huvuma unakopenda,
Yakakukumba ulipo, ukaacha randaranda,
Yakakupatia pepo, moyoni ukayafunda,

Mapenzi kama asali, ukauchonga mzinga,
Ukitaka kukabili, nyuki hawatakuzinga,
Penzi si kitu muhali, wewe usije jivunga,

Mapenzi kama shairi, yenye lugha yenye kina,
Ndiyo hayo ya bukhari, ni mapenzi yalo nona,
Yafaa yako nadhari, waziwazi nimenena,

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)