Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kuna kundi la watu ambao wanaiomba serikali ifungie twitter nchini kwa kudai kuwa twitter imeruhusu maudhui ya mapenzi ya jinsia moja. Hata hivyo, najiuliza ni mtandao gani ambao hauruhusu mapenzi ya jinsia moja kwa hoja hiyo kuwa na mashiko. Je ni kweli meta haruhusu maudhui ya mapenzi ya jinsia moja? Hapa naona kuna zaidi ya jambo hili ambalo wengi wameliingilia na kulilalamikia kana kwamba wanaongea ukweli.
Aidha sera ya twitter (X) imekuwa tu kwamba inaruhusu maudhui ya ngono, na maudhui ya ngono yanapatikana maeneo mbalimbali sio tu X, tena kwa muangaliaji wa ngono hawezi kukaa X kutafuta ngono ataingia mitandao stahiki.
Kwa hiyo hao vijana wanaoomba X au twitter ifungiwe, wanasababu gani haswa. Kama ishu ni maudhui ya mapenzi ya jinsia moja kwa nini wasiombe mitandao yote ifungiwe tuwe kama China tu?