Tanganyika ni nchi iliyofichwa chini ya mwamvuli wa Muungano. Watanganyika ni watu wenye tabia tofauti na Wazanzibari. Tumewaruhusu wazanzibari watutawale kwa kivuli cha muungano na sasa wamefikia hatua ya kujimilikisha maliasili zetu.
Kitendo cha kukodisha bandari kwa mkataba usio na ukomo na hata kuamrisha polisi watushughulikie pale tunapohoji yale tunayoona ni kinyume na katiba ya nchi yamedhihirisha jambo hili. (Rejea kauli ya waziri Masauni akiamrisha polisi watukamate na kutupiga pale tunapohoji maswala ya mkataba tata wa DP-World)
Wakati Wazanzibari wakiwa wamesimama imara kuulilia utambulisho wao kimataifa sisi Watanganyika tumelala usingizi wa pono. Hatutaki kudai wala hatujishughulishi kudai iliyo haki yetu. Kumbe tulidanganywa tangu tulipokuwa shule za msingi kuhusu muungano wa Tanganyyika na Zanzibar na kuunda Taifa jipya la Tanzania kinyume chake ni kwamba tuliuficha Utanganyika na kuuanzisha, kisha kuutukuza Utanzania ambao kwa sasa umekuwa ni sehemu ya anguko letu kama taifa.
Ni wajibu wetu sasa sisi kama raia wa Tanganyika kuendelea kudai uhuru kamili wa kujitawala, huku tukiamini kwamba Wazanzibari ni wenzetu na ndugu zetu katika muungano huu lakini hawana mamlaka ya kututawala ama kutuamulia cha kufanya katika ardhi yetu wenyewe. Viva Tanganyika, aluta continua.
View attachment 2683029