Ni muda muafaka sasa kwa Tume ya Ushindani Tanzania FCC kulimulika swala la uwekezaji wa Mo Dewji Simba

Ni muda muafaka sasa kwa Tume ya Ushindani Tanzania FCC kulimulika swala la uwekezaji wa Mo Dewji Simba

Wewe ni mtoto Mdogo sana, huna ulijuwalo.

Ruzuku ya serikali inatolewa na wezi wanaoibia serikali kodi hao unaowaona GSM na Mo Dewji.

Reginald Mengi alikuja macho juu Yanga baada ya kuujuwa ukweli akakaa pembeni.

Zamani kwa watu wa Mwanza ukitaka kadi ya Yanga unachukulia kwenye ofisini za Toto Africa Mwanza, kuna mengi usiyoyajuwa ukikua utaacha huu ujinga wa kuwaita hamnazo watu waliokuzidi akili kwa mbali.

Kama upo karibu na Michael Wambura muulize mbona siku hizi hana kiherehere cha kugombea vyeo Simba?
Mkumbushe jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikiongozwa na Ali Hassan Mwinyi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiongozwa na marehemu Idrisa Abdul Wakili miaka Ile ya mwishoni mwa 80s zilivyoingilia katika hukumu ya Mahakama ya kulipigia mnada Jengo la klabu ya Yanga kutokana na madeni sugu.
 
Hekaya za abunuasi na stori za ESOPO ZINAENDELEA
 
Mkumbushe jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikiongozwa na Ali Hassan Mwinyi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiongozwa na marehemu Idrisa Abdul Wakili miaka Ile ya mwishoni mwa 80s zilivyoingilia katika hukumu ya Mahakama ya kulipigia mnada Jengo la klabu ya Yanga kutokana na madeni sugu.
Hajui lolote huyo, anabwatabwata tu, ulishasikia tena hilo deni?
 
FCC ndio wanaokwamisha mchakato wa Simba kuendeshwa kisasa, sababu ni hiyo Simba ni timu ya serikali hawawezi kuikabidhi kwa watu binafsi.

Serikali iliipora Simba kutoka kwa Waarabu Sunderland na kuipa jina la kawawa Simba wa Vita na Karume ndio alitowa pesa ya Kujenga makao mkuu ya Simba Msimbazi kama alivyotowa pesa za Kujenga makao makuu ya Yanga.












Simba SC ni moja kati ya timu nne kongwe kabisa hapa nchini ikianzishwa mwaka 1936 jijini Dar es salaam. Zingine ni vinara Yanga SC 1935, African Sports 1936 na Coastal Union 1938.

Simba imepitia majina mengi toka kuanzishwa kwake mpaka sasa. Ilipoanzishwa mwaka 1936 iliitwa Queens jina lilidumu mpaka mwaka 1948 walipofanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza na wakati huo mkoa wa Pwani ulianzisha ligi maalumu iliyokuwa ikijiendesha kwa misingi bora ya kisasa.

Wakati huu ndio Simba ilianza kupata ufadhili unaoeleweka mfano jezi nzuri za kisasa na viatu wakati wenzao wakiwa bado wakilisakata kabumbu peku peku .

Simba walibadilishwa jina na kuitwa Eagles baada ya kuonekana jina la Queens linawaletea kebehi kwa watani wao wa jadi Yanga SC ambao kabla ya mwaka 1930 walijulikana ‘ New Young ‘.

Jina la Eagles yaani tai kwa lugha ya kiswahili halikudumu sana. Lilikaa kwa muda mchache sana na kubadilishwa kuwa Sunderland.

Hili ndio jina ambalo wengi wanalifahamu sana . Ni jina ambalo wekundu hawa wa msimbazi wana kumbukumbu nalo kubwa na ndefu kidogo.

Baada ya nchi kupata Uhuru mwaka 1961 na miaka minne baadae kuanzishwa ligi daraja la kwanza yenye sura ya kitaifa yaani ligi iliyoshirikisha timu zote za bara na visiwani, Sunderland ndio ilikuwa timu ya kwanza kubeba kombe la ligi hiyo mwaka 1965 na kulitetea tena kombe hilo mwaka 1966.

Hivyo katika historia Simba SC wakitumia jina la Sunderland waliweza kunyakua ubingwa wa ligi daraja la kwanza mara mbili kabla ya jina hilo kufa mwaka 1971 baada ya raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Karume kuwashauri kubadili jina kwa sababu ya maudhui yake kikoloni na ndipo jina la Simba SC lilipozaliwa.
 
Do your home work, ukitaka ukweli utakuja kuujuwa fuatilia kuanzia usajili wa Simba na Yanga utapata ukweli.

Upande wa Yanga GSM wanajuwa kila kitu ndio maana wamemuweka Eng Hersi asimamie maslahi yao wanajuwa vizuri Yanga haiwezi kumilikiwa na watu binafsi.
Sasa kosa liko wapi Mo kumuweka babra kisimamia maslahi yake pale simba? Nyie wapiga zumari tushawazoea mikelele yenu wakati hamna hata mia mfukoni
 
Wakuu Simba ni brand, siyo kikundi cha wahuni, na kila kilichopo Simba ni mali ya umma (wanachama). Hivyo kumpatia mtu hisa asilimia 49 kinyemela ni sawa na uhalifu.

Tume ya ushindani unapaswa sasa kuingilia kati hili suala la uwekezaji la huyu bwana, maana inavyoonekana mazingira yake ni ya kihuni.

Simba watuambie kama wameingia mkataba wa zaidi ya shilingi bilioni 20 na M bet inakuwaje umiliki wa asilimia 49 uwe na thamani ya bilioni 20 tu?

Lakini pia je Mo Dewji ni mmiliki wa kilabu ama mdhamini, maana jezi za kilabu zimejaa matangazo ya kampuni zake tanzu.

Wakuu ya kuzungumza ni mengi ila kwa hapa hapana, jamaa achunguzwe na watuambie je, ni kweli Klabu ya Simba inastahili kumilikishwa kwa mtu kwa thamani ya 20 bilioni?

NB. Ujenzi wa kiwanja wanachangia wanachama na Mohamed Dewji ameshaupatia tayari jina lake et MO Arena. Aibu kubwa hii watanzania.
SAWA ILA HAWATAKUELEWA
 
Back
Top Bottom